Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa
madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete
kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.
Balozi
wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan akizungumza baada ya kuzindua majengo ya
madarasa sita na ofisi moja ya walimu yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakistan
katika shule ya msingi Pakistan utete iliyopo kata ya Pera,kushoto kwake ni
mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani
Kikwete, amezindua Madarasa sita yenye yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakstani
kwa gharama ya shilingi milioni 30
Madarasa hayo sita na ofisi moja ya
walimu yamejengwa katika shule ya msingi Pakistan Utete iliyopo kata ya Pera,
Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
madarasa hayo, Mbunge huyo wa Jimbo la Chalinze aliwataka wananchi waache tabia
ya kusubiri kila kitu kufanywa na serikali na badala yake wawe mstari wa mbele
kujitolea katika shughuli mbali mballi za maendeleo.
Aidha amesema ofisi yake na halmashauri
wataendelea kuunga mkono juhudi za wafadhili na wadau mbalimbali wanaojitokeza
kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili zilizopo katika jimbo hilo
ikiwemo elimu.
Alisema baadhi ya wafadhili wanasaidia
endapo wanaona jamii husika ikichukua juhudi juu ya jambo fulani na kufikia
hatua mbalimbali .
Aliwataka wananchi wa Chalinze
kushirikiana na serikali, halmashauri na wafadhili wanaojitokeza ili
kukamilisha miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.
Aliongeza kwa kusema kuwa kipaumbele katika
Halmashauri ya Chalinze ni kuondoa changamoto zote zilizopo katika sekta ya
Elimu.
Ridhiwani alisema wakati marafiki wa
Pakistan wakiwezesha ukarabati huo,lakini halmashauri ya Chalinze imeshatenga
fedha kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo nane katika shule ya Pakistan Utete.
Aliongeza kwa kusema kuwa, wanajenga
matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mbala sanjali na madarasa mawili ya
shule ya msingi Makombe.
Ridhiwani alieleza,ujenzi wa matundu ya
vyoo utasaidia kuondoa kero ya uchafu wa mazingira ambapo baadhi ya wanafunzi
wamekuwa wakijisaidia ovyo maporini ,vichakani .
Akizungumzia msaada walioupata
kutoka kwa marafiki wa Pakistan, Mh. Ridhiwani aliwaomba marafiki hao
kuendeleza ushirikiano baina yao na Halmashauri ya Chalinze ili kufanikisha
mambo mbalimbali ya maendeleo.
Alitumia nafasi hiyo kumpongeza
mwenyekiti wa kitongoji Hussein Mramba na diwani wa kata ya Pera kwa jitihada
walizozichukua kusukuma jambo hilo.
Aidha, alimuomba Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Amir
Khan ,kuwasaidia ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa na mashine za kupima
magonjwa katika kituo cha afya Chalinze.
Balozi
wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan akizungumza baada ya kuzindua majengo ya
madarasa sita na ofisi moja ya walimu yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakistan
katika shule ya msingi Pakistan utete iliyopo kata ya Pera,kushoto kwake ni
mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete.
Kwa upande wake Balozi wa Pakistan hapa nchini,
Amiri Khan, alisema amefurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi hiyo na
Tanzania,na alishauri kuwepo na mahusiano kati ya wabunge wa Pakistan na
Tanzania.
“Nilipoambiwa kuja shuleni hapa ni km 120
kutoka Dar es salaam nikaona nije kutembea na kuona kilichofanyika, Nawapongeza
kwa kuanzisha ujenzi huu ili watoto wapate elimu”alisema Khan.
Alisema ili watoto hao wasome vizuri ni
vyema kukajengwa uzio katika shule hiyo ili kuweka usalama zaidi na kwamba
wanaweza kusaidia kuujenga.
Balozi huyo,aliahidi na kukubali ombi la
kusaidia mashine na vifaa vya kituo hicho cha afya lakini kwasasa wanachotakiwa
kufanya ni kuandika maombi ya msaada huo.
Balozi
wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan
Kikwete,wakikagua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule
ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki
wa Pakistan
Balozi
wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan
Kikwete,wakiingia katika lango kuu la majengo ya madarasa sita na ofisi
moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya
Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete kushoto akiagana na balozi wa Pakistan
nchini Amir Khan baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya
walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa
ufadhili wa marafiki wa Pakistan.
No comments:
Post a Comment