Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani kikwete katikati na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Chalinze, Edes Lukoa kulia wakikabidhi Pikipiki kwa watumishi 10 wa
Halmashauri hiyo na hivyo kufanya jumla ya watumishi waliopewa pikipiki kufikia
14.
Mbunge
wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa Halmashauri ya Chalinze imejipanga
kuwaondolea adha ya usafiri watumishi wake kwa kuwapatia pikipiki.
Alisema
awali walianza kuwapa pikipiki maafisa Mifugo wanne na baada ya kukusanya nguvu
ya kutosha wamewapatia pikipiki watendaji hawa 10 ili kukamilisha idadi ya
watumishi 14 katika halmashauri.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, awamu inayokuja ni kuwaangalia Watendaji Kata zote ili kuweza
kuwafikia wananchi waliowachagua na kusikiliza shida zao na kuzitatua.
No comments:
Post a Comment