Jumla ya skauti wapatao 200
kutoka jimbo la Hamshire Uingereza wapo nchini Tanzania kwa ziara ya kazi za
jamii pamoja na skauti wenzao wa Tanzania.
Skauti hao wamekuja nchini kwa ajili ya kufanya kazi za jamii ambapo
wamejitolea kukarabati Kambi kuu ya Mafunzo ya Skauti iitwayo Bahati ambayo ipo
mkoani Morogoro nje kidogo ya mji huo.
Ziara hiyo ambayo itachukua zaidi ya mwezi mmoja kukarabati eneo
hilo la kambi, na baada ya hapo watatembelea maeneo mengine ya Kilosa, Ifakara,
na Mikumi kabla ya kurejea nchini kwao Uingereza.
Kazi za kujitolea kwa vijana Skauti ni mojawapo ya shughuli zao za kila
siku kusaidia watu siku zote kama Kanuni za Skauti zinavyosema.
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la Skauti kutoka Uingereza
kutembelea Tanzania.
Wakiwa nchini Tanzania skauti hao kutoka nje wanashirikiana na wenyeji
wao Chama cha Skauti Tanzania, kutoka Makao Makuu D’salaam na wengine wa mkoani
Morogoro.
HIDAN .O. RICCO.
KAMISHNA MKUU MSAIDIZI
MAWASILIANO NA HABARI
(0673 019112)
No comments:
Post a Comment