Jeshi la Polisi mkoani Pwani limesema limejipanga kudhibiti Bandari bubu
zilizopo Bagamoyo ili kukomesha Biashara ya kusafirisha kutoka nje ya nchi
kinyume na utaratibu,
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa
wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Jonathan Shanna, alisema Bagamoyo
pekee ina Bandari bubu 18 na kwamba miongoni mwa njia zinazotumika kupitisha wahamiaji
wa kigeni bila ya kufuata utaratibu ni pamoja hizo.
Aidha, Kamanda Shanna alisema Jeshi la polisi mkoani Pwani limejipanga
kudhibiti njia zote za panya zinazotumika kupitisha magendo ya aina mbalimbali.
Kamanda Shanna alitoa kauli hiyo wakati akitoa Taarifa kuhusu wahamiaji 72
walioingia nchini kinyume cha sheria ambao walikamatwa hivi karibuni katika
shamba la Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO)huko Vigwaza wilaya ya kipolisi
Chalinze.
Kamanda Shanna ,amesema kuanzia sasa.watataifisha mali zote za watu
wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.
Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu
kusafirisha wahamiaji hao kwani navyo vitataifishwa .
Alisema wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu
watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji fedha
na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.
Kamanda Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za
wale watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.
Alisema sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini
hivyo itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa adhabu
zote na kufungwa .
Kamanda Shanna ,alisema taarifa ikifika kwao kuwa wanafungwa na kupewa
adhabu kali ndipo wataacha kuingia nchini kwani watajua Tanzania sio mahala pa
mchezo wala kukimbilia.
“Hii kuwakamata kuwapiga faini na kuwarudisha kwao ndio maana wanafanya
mchezo mchezo kukimbilia huku,ukiwapiga faini wanakwenda wanarudi ni mchezo wa
kuigiza”alisema .
Kamanda Shanna alielezea kwamba,Tanzania ina sheria zake endapo sheria
zitawabana wahamiaji hao na kukoma kugeuza nchi kuwa lango lao la kupita kwenda
nchi jirani ikiwemo Afrika ya kusini.
Hata hivyo ,kamanda huyo alisema wahamiaji waliokamatwa wameshawafikisha
ofisi ya uhamiaji mkoani Pwani na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Pamoja na hilo,Kamanda Shanna alisema wanafanya oparesheni kusaka
wahalifu mbalimbali ,zoezi ambalo ni endelevu.
No comments:
Post a Comment