Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani
kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya kata ya Kiwangwa, ambapo kulia ni Diwani wa kata ya Kiwangwa akiwa na Mtendaaji wa kata yake wakipokea vifaa hivyo kwa niaba ya timu yao.
................................................
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani
kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki
mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu kutoka kata zote za
wilaya ya Bagamoyo.
Sherehe hizo zilizofanyika kata ya Kimange
zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na
watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya,
Mh. Alhajj, Majid Mwanga, ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo
akishirikiana na wabunge wa majimbo yote mawili ya Bagamoyo na Chalinze pamoja na DAWASCO Bagamoyo, lengo likiwa ni kuihamasisha jamii ya wana Bagamoyo
kuendeleza usafi wa mazingira.
Pamoja na kugawa jezi hizo, mbunge wa Chalinze
aliziahidi timu za Jimbo la Chalinze kwamba mshindi wa pili wa mashindano hayo
atapatiwa Pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote Tatu za juu.
Kombe hilo la Mazingira Wilayani Bagamoyo
linashirikisha timu 28 ambazo kati ya hizo 11 kutoka kata za jimbo la Bagamoyo,
15 kutoka kata za jimbo la Chalinze na 2 Bodaboda wa Chalinze na Bagamoyo na
kufanya idadi ya timu kuwa 28.
Kwa udhamini wa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo pamoja
na DAWASCO Bagamoyo, Mshindi wa kwanza atapatiwa Pikipiki ya miguu mitatu (TOYO)
ambayo itawasaidia katika uzoaji wa taka katika kata husika.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani
kikwete, watatu kushoto akifurahia jambo pamoja na viongozi wengine, wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya kata ya Miono ambapo Diwani wa Kata ya Miono, Mh. Juma Mpwimbwi ameshika vifa hivyo pamoja na wajumbe wake kutoka kata ya miono, wa kwanza kushoto, ni Diwani wa kata ya Talawanda ambae pia ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mh. Saidi Zikatimu na wa nne kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhajj, majid Mwanga.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhajj, majid Mwanga, akionesha moja ya jezi zilizotolewa, pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, mh. Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo kwa Diwani wa kata ya Mbwewe, Mh. Ramadhani Mahamba, wa nne kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhajj, majid Mwanga.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo.
No comments:
Post a Comment