Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA, Mwajuma
Saidi Masaigana, kushoto akipokea tuzo maalum kutoka kwa Umoja Group ya nchini
Ujerumani, mara baada ya kutembelea shuleni hapo na kufurahishwa na namna shule
hiyo inavyowaandaa watoto katika kupata Elimu bora huku wakiwa katika mazingira
mazuri ya kujifunzia, anaemkabidhi zawadi hiyo kulia ni Mwenyekiti wa umoja
Group, Veronika Tereh.
Baadhi ya wanakikundi cha umoja Group kutoka
nchini Ujerumani, wakiwa kwenye jukwaa ambapo waliimba wimbo unaohimiza umoja
kwa lugha kiswahili, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi
MWASAMA, mara walipotembelea shuleni hapo, Mwenye shati ya njano katikati ni
Mwenyekiti wa umoja Group, Veronika Tereh.
Mwenyekiti wa umoja Group, Veronika Tereh.
Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA, Mwajuma
Saidi Masaigana, akiwa na wageni waalikwa meza kuu wakati wa kuwakarisha wageni wa Umoja Group kutoka nchini Ujerumani walipotembelea shuleni hapo.
Sehemu ya wgeni kutoka nchini Ujerumani wakiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa na wanafunzi wa shule ya MWASAMA.
wageni wa Umoja Group kutoka nchini Ujerumani wakipata vinywaji mara kumaliza kufanya mazungumzo na wenyeji wao walipotembelea shule ya msingiMWASAMA iliyopo mjini Bagamoyo.
Afisa Utamaduni wilaya ya Bagamoyo, Hamisi kim,
(kushoto) alipowasili katika shule ya msingi MWASAMA ili kushiriki hafla fupi
ya kuzungumza na wageni wa kikundi cha Umoja Group kuoka nchini Ujerumani
walipotembelea katika shule ya MWASAMA, kulia ni Mratibu wa shughuli hiyo,
ambae pia ni mjumbe wa bodi ya shule, Hamza Mfaume.
Mkurugenzi wa KAYA FM. RADIO ya mjini bagamoyo,
Marie Shaba, akizungumza na wageni kutoka nchini ujerumani katika hfla fupi ya
kuwapokea iliyofanyika shule ya Msingi MWASAMA mjini Bagamoyo.
Mjumbe wa kamati ya CCM wilaya ya Bagamoyo,
Mwinyi Hashim Akida, akizungumza na wageni hao, kushoto ni Mwalimu John Mponda
kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Wageni hao walipata fursa ya kutembelea eneo la
shule ambapo ndani yake walijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shule
hiyo ikiwemo ufugaji wa Samaki kama hapa wanavyoangalia Samaki waliofugwa
kwenye Bwawa.
No comments:
Post a Comment