Kocha
Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia
klabu ya Yanga.
Zahera amechukua rasmi mikoba ya
Mzambia aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kimyakimya
kurejea kwao Zambia
katika klabu yake ya zamani, Zesco United.
Zahera alichelewa kusaini mkataba
na Yanga kutokana na majadiliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo, lakini
sasa wamefikia mwafaka na ameamua kuweka kandarasi hiyo itakayomalizika mwaka
2020.
Licha ya kusaini mkataba huo,
Katibu Mkuu wa Yanga, Biniface Mkwasa, mapema leo asubuhi alieleza kuwa Zahera
ameondoka nchini kwenda kwao Congo
kwa majukumu ya kukitumikia kikosi cha timu ya Taifa ya Congo.
Aidha, mkanganyiko umekuja mara
baada ya kusema kuwa Zahera ameondoka akiwa bado hajasaini mkataba kutokana na
makubaliano kutofikia mwafaka baina ya pande mbili kati ya Zahera na uongozi.
No comments:
Post a Comment