Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo(aliyeinama) wakati alipotembelea
maduka ya bidhaa ya mafuta ya kupikia na sukari ,Loliondo ,Mailmoja ,Mjini
Kibaha,(Wa pili kutoka kulia) ni kamanda wa polisi wa mkoa huo , (ACP) Jonathan
Shanna na wa kwanza kushoto mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoani Pwani
,Abdallah Ndauka.
..........................................
Na
Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI
mkoani Pwani,imewahakikishia wananchi kuwa inawasimamia wafanyabiashara wa
mafuta ya kupikia ,washushe bei ya bidhaa hiyo ambayo kwasasa inauzwa lita moja
sh.5,000 kutoka sh.3,200 iliyokuwa ikiuzwa kipindi cha nyuma.
Aidha
imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa sukari na mafuta hayo, ambao watajaribu
kuficha bidhaa hizo kwa lengo la kujitajirisha haraka haraka baadae kwa
kupandisha bei na kudai atakaefanya hivyo atakiona.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo aliyasema
hayo wakati alipotembelea maduka ya bidhaa hizo ,Loliondo ,Mailmoja ,Mjini
Kibaha huku akiwa ameambatana na kamanda wa polisi wa mkoa huo , (ACP) Jonathan
Shanna .
Alisema
Mei 16 mwaka huu,waliamua kutembelea baadhi ya magodauni na maduka ya bidhaa
hizo ambapo wamejiridhisha kwa kukuta sukari ikiuzwa bei nzuri na maeneo
mengine wakishusha madumu ya mafuta kwa ajili ya kuuzia walaji.
Ndikilo
alieleza kwamba ,hategemei kuona wala kusikia kuna mfanyabiashara atakaefanya
kitendo hicho ili bidhaa hizo ziwe adimu .
“Kama
yupo mfanyabishara atakaejaribu kuficha mafuta na sukari kwa uroho wa fedha
,atakumbana na mkono wa sheria na hatutosita kumchukulia hatua za kisheria”
“Serikali
inachunguza wote watakaoficha bidhaa hizo ,na jeshi la polisi mkoani hapa chini
ya kamanda Shanna linaendelea na misako mbalimbali na kusimamia suala hili na
wamejipanga”alisisitiza Ndikilo.
Akizungumzia
sukari ,Ndikilo ambae pia ni mkuu wa mkoa huo,alisema bidhaa hiyo ilikuwa
ikiuzwa 2,600 kwa kilo lakini imeshuka hadi 2,400/2,300 .
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara mkoani Pwani, Abdallah Ndauka aliwataka wafanyabiashara
watoe huduma kama inavyostahili na kwa wakati.
Aliwaomba
wazalishaji wa bidhaa viwanda kuzalisha na kusambaza kwa wingi bila
kuwakwaza wananchi.
Ndauka
alisema kuwa,kama chama watawashughulikia wafanyabiashara watakaokwamisha jambo
hilo na kuwaasa wawe sehemu ya kutoa huduma stahiki hasa mwezi huu mtukufu wa
Ramadhani.
Nae
kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ,Shanna alisema wameyabeba maagizo yaliyotolewa
na kusema wanajua magodauni,store na maduka yote yanayouza bidhaa hizo hivyo
asithubutu mfanyabiashara kulijaribu jeshi hilo.
Shanna
alielezea,ameshayapokea maelekezo kazi yake kubwa ni utekelezaji wa vitendo
kwani wanaintelijensia ya kutosha.
Kwa upande
wao wafanyabiashara akiwemo Kassim Haji ,alisema mafuta ya kupikia yalipotea
lakini kwasasa kuanzia Mei 16 yameanza kuingia na kwa yeye anatarajia kupokea
madumu 600.
Alisema
wanatarajia kushusha bei baada ya kuanza kupelekewa mafuta kwani awali kulikuwa
na shida bandarini na anaahidi kushusha gharama ya bidhaa hiyo.
Nao
baadhi ya wananchi waliokuwepo soko la Loliondo kwa ajili ya kujinunulia
vyakula na bidhaa mbalimbali akiwemo Zulfa Rashid ,alisema bidhaa inayowaumiza
ni mafuta ya kupikia.
Aliomba
mafuta hayo yashushwe bei kwani yanauzwa kwa sh,5,000 kwa lita moja fedha
ambayo ni kubwa na maisha ni magumu hasa kuelekea kipindi cha mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
“Tunaomba
gharama zishushwe ,serikali isimamie suala hilo,na tunashukuru mkuu wa mkoa
kuja kuzungumza na sisi ,pamoja na kutuhakikishia bidhaa hizo zitashushwa bei.
Zulfa
alisema, wengi wao wanatumia nazi na kuacha kununua mafuta kutokana na gharama
kupanda tofauti na zamani.
No comments:
Post a Comment