Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wananchi mkoani humo kuacha
kuvamia maeneo hifadhi za misitu ili kuruhusu uoto wa asili kwa manufaa ya
taifa.
Mhandisi
Ndikilo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kukagua Hifadhi ya Msitu wa Zigua
ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imevamiwa.
Akizungumza
mara baada ya kujionea hali ilivyo kwa sasa katika msitu huo Mkuu huyo wa Mkoa
alisema baada ya kuwaondoa wavamizi katika hifadhi za misitu za mkoa wa Pwani
hali za misitu hiyo imerejea kama kawaida na
kwamba sasa misitu hiyo imeanza kupendeza.
Alisema
kufautia kurudi kwa hali ya kawaida katika Misitu hiyo Mkuu huyo wa Mkoa
alisema wananchi mkoani humo wanapaswa kuwa walinzi wa misitu hiyo na kwamba
waache kuvamia na kufanya shughuli za kibanadamu.
Aliitaja
misitu hiyo iliyopo Mkoa wa Pwani kuwa ni Msitu wa Zigua, Msitu wa kazi
mzumbwi, na Msitu wa Ruvu kusini
Akizungumzia
umuhimu wa Msitu wa Zigua alisema msitu huo ni mapitio ya wanyama kutoka mbuga
ya wanyama Saadani kuelekea Mikumi na Mbuga Selou
Aidha,
aliongeza kwa kusema kuwa, Msitu huo ndio unaweza kuhifadhi mai ya mto wami
ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ya binadamu na wanyama katika hifadhi
ya wami mbiki iliyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya
mashariki Caroline Malundo alisema kwa sasa Msitu huo umerejea katika hali yake
ya kawaida na kwamba hata wanyama waliokuwa wametoweka wameanza kurejea.
Alisema
oparesheni ya kuwaondoa wavamizi katika msitu huo iliyofanywa kwa kushirikiana
na kamati za ulinzi na usalama za wilaya tatu ambazo ni Handeni, Bagamoyo na
Kilindi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba mpaka sasa hakuna wavamizi
ndani ya msitu huo.
No comments:
Post a Comment