Wachezaji wa Timu ya Mpira wa miguu ya Stendi Fc ya mjini
Bagamoyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga (mwenye fulana ya punda milia) wakati wa kuwaaga kuelekea kwenye mashindano ya kuwania kuingia ligi Daraja la pili yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro.
.............................
Timu
ya Mpira wa miguu ya Stendi Fc ya mjini Bagamoyo imeingia kwenye kinyang'anyilo
kutafuta ushindi wa kuingia ligi daraja la pili.
Timu
hiyo ya Bagamoyo ni timu pekee, ambayo
inawakilisha mkoani Pwani katika
mashindano hayo ambapo imeondoka kuelekea wilaya ya Moshi mkoani kilimanaro.
Katika
kufanikisha safari ya vijana hao wawakili wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga amepokea fedha taslimu shilingi milioni tano laki
mbili na elfu sabini na tano 5,275,000 kutoka kwa wafugaji wa Halmashauri ya
Chalinze ili kuiwezesha timu hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kupokea fedha hizo Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru wafugai hao
kwa uzalendo wao kwani wameweza kuonyesha umoja wao kwa timu hiyo.
Miongoni
mwa wadau walioweza kuchangia timu hiyo ni pamoa na Hifadhi ya Taifa Saadan
ambapo waliweza kuchangia Jezi pea 3 kwa kila mchezaji.
Aidha,
Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuisadia timu
hiyo ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Alisema
timu hiyo ina uwezo mkubwa wa mpira hivyo ni matumaini yake kuwa itarudi na
ushindi ili iweze kupnda daraa kutoa daraja la tatu kwenda la pili.
Aliongeza
kuwa, ili timu iweze kufanya vizuri inapaswa kutizamwa kwa umakini katika
mahitaji yake hasa inapokuwa nje ya nyumbani kwake ambapo wachezai na viongozi
wa timu wasiwe na mawazo ya nyumbani na badala yake wacheze mpira vizuri na
kurudi na ushindi nyumbani.
Kwa
upande wake Nahodha wa timu hiyo ya Stend FC Soudi Abdalla Dondola lisema
wananmshukuru Mkuu wa wilaya kwa kuwapa msada mkubwa wa kuwawezesha kufanya
safari yao.
Akizungumzia
namna walivyojipanga katika mchezo Dondola alisema timu iko vizuri na kwamba
mashabiki wa Mkoa wa Pwani wategemee kuwa timu yao itaibuka na ushindi.
Kocha
Mkuu wa timu hiyo Sheikh Abdallaah Sheikh alisema timu yake iko vizuri na
kwamba wameipanga kushiriki mechi zote tano za kundi hilo
Alisema
lengo ni kurudisha ushindi Bagamoyo na kuifanya timu hiyo uweze kusonga mbele
mpaka kufikia ligi daraja la kwanza.
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa miguu ya Stendi Fc ya mjini Bagamoyo wakiwa katika harakati za kuanza safari.
Muwakilishi
wa Hifadhi ya Tifa ya Saadan akimkabidhi jezi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
kwaajili ya timu ya Stendi FC.
Wafugaji
wa Halmashauri ya Chalinze wakimkbidhi Fedha taslimu Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
kwajili ya timu ya Stendi FC
No comments:
Post a Comment