Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto Daniella
Wilfred Pallangyo mwenye umri wa miaka 8 ambaye ana matatizo ya kichwa kikubwa
wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa
na Ubalozi wa Kuwait
kwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa kuwait nchini
Mhe. Jasem Al Najem wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa
watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
............................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema
uboreshaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kama MOI, zitaipunguzia
Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo kutekeleza azma ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati wa kupokea vifaa vya Chumba Cha Upasuaji wa
Watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI) leo
tarehe 15 Mei, 2018.
“
Aidha kwa namna ya kipekee nakushukuru Mheshimiwa Balozi wewe binafsi na
Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano ambao mnaendelea kuipatia Serikali yetu ya
awamu ya Tano katika Sekta mbalimbali za maendeleo lakini hasa hasa katika
sekta ya afya” alishukuru Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais amesema kuwa Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem amekuwa mstari wa
mbele katika kuendeleza sekta ya Afya hapa nchini ambapo leo wamesaidia vifaa
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 258 ambavyo vitaiwezesha Taasisi
kuimarisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na
mgongo wazi.
Makamu
wa Rais amesema msaada huo utaiwezesha Taasisi kuwa na chumba cha upasuaji
ambacho kitakuwa maalum kwa watoto tu, hivyo idadi ya wagonjwa watakaopata
huduma ya upasuaji itaongezeka kutoka 500-700 kwa mwezi, kufikia zaidi ya
wagonjwa 1000 kwa mwezi na watahudumiwa kwa haraka zaidi.
Wakati
huo huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Faustine Ndugulile amesema Tanzania iatendelea kuimarisha uhusiano na
nchi ya Kuwait kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada haswa msaada
inayohusu sekta ya afya.
Balozi
wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem amesema kuwa Wananchi wa Kuwait wana
mapenzi makubwa na Watanzania na kuahidi wataendelea kutoa msaada.
No comments:
Post a Comment