Wednesday, May 23, 2018

WANAWAKE BAGAMOYO WAPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI.


Wanawake wa Bagamoyo wamepewa elimu ya ujasiliamali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Semina hiyo ambayo imeandaliwa na ... ililenga kuwajengea uwezo katika shughuli zao katika uzalishaji wa bidha mbalimbali.

Aidha, kinamama hao wametakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kukabiliana na ushindani wa soko.

Muwezeshai wa semina hiyo alisema ni lazima kina mama waiamini kile wanachofanya kwani kuiamini ni njia moja wapo ya kufikia malengo.

Kwa upande wao wanawake hao wajasiliamali wilayani Bagamoyo wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuzalisha bidhaa zao na kudhindwa kufikia malengo wanayojiwekea.

Walisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya ujasiliamali hali inayopelekea kinamama wengi kufanya kazi zao chini ya kiwango.

Waliongeza kwa kusema kuwa upatikanaji wa malighafi ni tatizo linalowakwamisha wengi kwakuwa malighafi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya juu au kukosekana kabisa na hatimae mjasiliamali anakata tamaa ya kuendelea na uzalishaji.

Kupitia semina hiyo kinamama hao wameiomba serikali kuwajengea mazingira mazuri wajasiliamali wanawake ili waweze kumudu kuzalisha bidhaa zao ambazo ndio msingi wa maisha yao na familia zao.

Awali akifungua semina hiyo, Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo Erica Yegela aliwataka kinamama kuwa kitu kimoja ili kufikia malengo wanayojiwekea

Alisema ni vyema wakawa kwenye vikundi ili kuweza kupata msaada ikiwemo mikopo ambayo itawasidia kuendesha shughulizao za ujasiliamli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi Bagamoyo Tedy Davis alisema tatizo linalowakwamisha wajasiliamli wananwake ni kukosa mitaji hali inayopelekea kushindwa kuzalisha bidhaa.

Alisema ipo mikakati mingi ya kuwawezesha wanawake Bagamoyo ili wajikwamue kiuchumi lakini utekelezaji wa mikakati mingi unahitaji fedha.
 
 
Washiriki wa  mafunzo hayo wakifuatilia kwa karibu.
 



No comments:

Post a Comment