Naibu
waziri wa Nishati, Mh. Subira Mgalu amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya
uongozi wa Dkt. John Magufuli imedhamiria kufikisha umeme kila kijiji ili
kuwaondolea adha wananchi walikosa huduma ya umeme kwa muda mrefu.
Naibu
waziri huyo wa Nishati ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani
aliyasema hayo katika ziara yake Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo
ambapo aliweza kuzindua miradi ya umeme vijijini REA kwa kuwasha umeme katika
vijiji kadhaa vya Halmashauri hiyo.
Aidha,
alisema ni fusa kwa wananchi sasa kujitokeza kuchukua fomu na kulipa gharama ya
shilimngi 27,000 kwaajili ya kuunganishiwa.
Alisema
uzinduzi wa miradi hiyo ya umeme ni utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na
serikali ya awamu ya tano katika kampeni za uchaguzi na kwamba kilichobaki sasa
ni utekelezaji tu.
katika
hatua nyingine Naibu waziri huyo amewashukuru wadau wa Elimu katika Halmashauri
hiyo wakiongozwa na Mrs Barbara na Wentworth Africa Foundation kwa msaada wao
walotoa katika Sekondari ya wasichana Mandela ambapo waliweza kukabidhi taulo
maalum kwaijili ya matumizi ya wasichana na kila msichana amepata Taulo Za
kutumia Mwaka Mzima Kwa Wasichana Mia Tano Hamsini.
Wakati
huo huo Naibu waziri huyo wa Nishati aligawa Taa za sola kwa Zahanati ambazo
hazijafikiwa na umeme ili kuwarahishia kina mama wakati wa kujifungua.
Naibu waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akiwa ziara katika vijiji vya Chalinze ambapo aliweza kuwasha umeme katika vijiji vya Hondogo na Saleni pmoa na kugawa Taa za sola katika Zahanati ya Mihuga.
Naibu
waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani akikabidhi Taulo maalum kwaijili ya matumizi ya wasichana Kwa Shule ya
Sekondari ya Wasichana Mandela ambapo kila msichana amepata Taulo Za kutumia
Mwaka Mzima Kwa Wasichana Mia Tano Hamsini, Msaada
huo umetolewa na Mrs Barbara na Wentworth Africa Foundation, Wadau hao wa Elimu Pia wameahidi kufadhili
ujenzi wa Maktaba.
Mh. Subira Mgalu amekabidhi, Mabox ya Vitabu Kwa Maendeleo ya Shule.
Naibu
waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa katika zoezi la kugawa Taa za solar Kwa
ajili ya Wadi za kuzalishia Kina Mama Kwa ajili ya Zahanati za Mihuga ,
Masimbani na Kweikonje Maeneo ambayo hayana MiundoMbinu ya Umeme.
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa kijiji cha Hondogo kata ya Miono Halamshauri ya Chalinze ambapo aliweza kuzindua mradi wa umeme viijini REA ambapo kijiji hicho sasa kimepata umeme.
No comments:
Post a Comment