WAZIRI wa Habari, Utamaduni,
sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika Kilele cha Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini .
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma , Katibu wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF) Nevile Meena alisema mada mbalimbali zitakazojadiliwa ni pamoja
na changamoto zinazovikumba vyombo vya habari katika kipindi cha miaka 27
tangu Azimio la Windhoek, Namibia, lilipopitishwa linalohusu uhuru wa vyombo
vya habari.
Akieleza
zaidi alisema, Kilele cha Maadhimisho hayo kitafikiwa
kesho, Mei 3, mwaka huu, mkoani Dodoma, ambapo siku moja kabla kutakuwa
na majadiliano kuhusu hali ya vyombo vya habari nchini ambayo yatafunguliwa na
Spika wa Bunge, Job Ndugai.
“Tutapata
Wakati muafaka wa kujadili mada kuu ya changamoto zetu, pia kutakuwa na mada
nyingine zitakuwa zinaendelea katika vikundi, ikiwemo inayohusu mitandao ya
kijamii kama inatakiwa kudhibitiwa au watumiaji ndio wajidhibiti wenyewe,”
alisema Meena.
Pamoja
na hayo alisema kutakuwa na mada kuhusu unyanyasaji wa kingono ndani ya vyombo
vya habari, na kuona kama suala hilo bado ni kikwazo hasa kwa waandishi
wanawake kupata nafasi za juu kwenye vyombo vya habari.
Aidha
Katibu huyo wa TEF alisema, kutakuwa na mada kuhusu usalama wa waandishi wa
habari, ni kiasi gani waandishi wanakuwa salama wanapofanya kazi zao katika
maeneo mbalimbali.
“Suala
la haki za kupata habari, japo limeingizwa kwenye sheria tangu mwaka 2016 na
kanuni zake Februari mwaka huu, na namna gani mwandishi anaweza kudai haki
hiyo,” alisema.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Klabu za Waandishi Tanzania (UTPC), Jane Mihanzi aliyataja
maadhimisho hayo kuwa ni fursa kwa wadau wa habari kujadili namna vyombo vya
habari vilikotoka, vilipo na wapi vinaelekea.
” Sisi
kama wadau wa habari tunaotambua na kuwajali wananchi kupata habari, tumekuwa
tukisaidia waandishi kuwapamafunzo na vifaa vya kazi,”alisema.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Razia Mwawanga
alisema kupitia maadhimisho hayo wanahabari na jamii kwa ujumla wataelewa
umuhimu na wajibu wa kuwajibika.
Alisema,japo
kuwa taaluma hii ina vikwazo vingi kuna ,waandishi watapaswakuwajibika kwa
kujitolea ikiwa ni pamoja na kuhamasika kuacha kuandika habari kwa mazoea
na bafala yake wajikite katika kuandika habari zenye maslahi za kueleza wajibu
wa serikali kwa umma na umma kwa serikali yao.
Hata hivyo alisema fani ya uandishi habari inapaswa kujikita katika maadili ya
uandishi bora kwa kuzingatia vigezo weledi na si vinginevyo kwani hii
itasaidia ukuwaji wa fani hiyo hapa nchini na kuondokana na uandishi wa
kimazoea katika kutekeleza majukumu ya wanahabari ya kila siku.
No comments:
Post a Comment