Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Baraza Maalum la kufunga mwaka
2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Baraza hilo limehudhuriwa na Maafisa na
Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya, Chuo cha Magereza
Kiwira na Chuo cha Ufundi Mbeya ambapo Baraza hilo limefanyika leo Desemba 31,
2017 katika Viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya.
Baadhi
ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya
Mkoa wa Mbeya wakisikiliza hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(hayupo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na
kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Wakuu
wa Magereza yaliyopo Mkoani Mbeya wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelekezo ya
Kamishna Jenerali wa Magereza aliyoyatoa katika Baraza Maalum la kufunga mwaka
2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Mkuu
wa Magereza Mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kijida
Mwakingi akitoa taarifa fupi ya Mkoa wake katika Baraza Maalum la kufunga mwaka
2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Naibu
Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akitoa ufafanuzi wa masuala yahusuyo
Divisheni ya Huduma za Urekebishaji mbele ya Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) katika Baraza la kufunga mwaka 2017
na kuukaribisha mwaka mpya 2018 (wa kwanza kushoto) ni Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza. Baraza hilo limefanyika katika
Viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya.
Mkuu
wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu katika Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Chacha Binna akitolea ufafanuzi kuhusiana na masuala ya
madeni ya watumishi yaliyoulizwa na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo Mkoani
Mbeya(hawapo pichani) katika Baraza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua gwaride la
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kabla ya kuhutubia Baraza Maalum la
Maafisa na Askari wa Jeshi hilo lililofanyika katika Viwanja vya Magereza
Mkoani Mbeya leo Desemba 31, 2017
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment