Jukwaa la wanawake wilaya ya Bagamoyo linaandaa
maonyesho kwa wajasiliamali ili kutafuta fursa zilizopo katika jamii.
Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi
wilaya ya Bagamoyo Teddy Alban Davis amesema wamefikia uamuzi wa
kufanya maonyesho hayo baada ya kufanya utafiti wajasiliamali wanawake katika
kata 11 za Halmashauri ya Bagamoyo.
Alisema katika vikundi vya wajasiliamali wanawake
wilayani Bagamoyo vipo vyenye uezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na zenye
kuvutia lakini watambuliki.
Teddy alisema kwa kutumia maonyesho hayo
wajasiliamali watapata nafasi ya kuonyesha bidhaa zao na kutambua fursa
zilizopo kupitia watu watakaohudhuria katika maonyesho hayo.
Aidha, alisema mwenyekiti huyo alitoa wito kwa
wajasiliamali wa Bagamoyo kujitokeza kwa wingi ili kupata nafasi ya kuonyesha
bidha zao.
Mwenyekiti huyo aliwataka wajasiliamali wanawake
kuwasiliana na ofisi za kata ili kupata maelekezo ya kushiriki maonyesho hayo.
Alisema maonyesho hayo yatafanyika siku ya tarehe
20-25 Desemba 2017 katika uwanja wa
Mwanakalenge ambapo Taasisi mbali mbali zitakuwepo kama TBS, TFDA, SIDO NK.
No comments:
Post a Comment