Thursday, December 7, 2017

WAZIRI WA MAJI AKAGUA MRADI WA MAJI BAGAMOYO

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe, (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Majid
Mwanga, (wapiili kulia) na Wakandarasi kutoka kampuni ya India ya
WAPCOS.
Mhe. Mhandisi Kamwelwe, akizungumza jambo na Mhe. Ridhiwani
Kikwete, walipotembelea chanzo cha Maji Mto Wami.
.......................

WAZIRI
WA Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe ametembelea na
kukagua maendeleo ya ujenzi Mradi wa maji awamu ya tatu ya upanuzi wa chanzo na mtandao wa maji wa Chalinze mkoani Pwani leo Desemba 6, 2017.

Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), upanuzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa matenki na ulazaji wa mabomba, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya za Mradi.

“Mradi huu unahusisha  upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji wa Chalinze ambao chanzo chake ni Mto Wami na lengo ni kuongeza
uzalishaji kufikia mita za ujazo Elfu Tisa (9000) kwa saa kutoka mita za ujazo
Mia Tano (500) kwa saa.” Amefafanua Mhandisi Kamwelwe.
 

Akifafanua
zaidi Mhandisi Kamwelwe amesema, Mradi pia unahusisha ujenzi wa

Matrenki 19, ulazaji wa mabomba ya ukubwa tofauti wenye urefu wa kilomita 1,022, ujenzi wa vizimba vya kuchotea maji 351 katika  vijiji na


vitongoji vya Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo Mkoani Pwani.

“Mradi huu ni Mkubwa na unahusisha pia baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga na Morogoro katika wilaya za Handeni na Ngerengere.” Ameongeza Waziri huyo. 

Aidha
Mheshimiwa Waziri, alisema Wananchi wa maeneo yatakayofaidika na Mradi huo ambao ni Mkubwa ni pamoja na wakazi wa Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga mji na vitongoji vya Chalinze, na baadhio ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha Mkoani Pwani, wakazi wa maeneo ya Kizuka A na B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A

na B Mkoani Morogoro. 

Maeneo


mengine yatakayojengwa matenki ni pamoja na Pera, Pingo, Bwilingu, Msoga, Diozile, Lugoba, Mindutulieni, Saleni, Mazizi, Msata, Kihangaiko, Kilemera, Hondogo, Miono North 3, Kimange, Rupungwi na Manga.
Kati ya matenki hayo 19 mojawapo ni tenki kuu la Mazizi lenye uwezo wa kuhifadhi lita Milioni 2, kukamilika kwa ujenzi wa tenki hiulo kutafanya kuwa tenki kubwa zaidi kuliko yote Mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa Mhandisi Kmwelwe, Mradi utrakapokamilika utagharimu dola za KImarekani Milioni 41.36 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim yta nchini humo. 

Hata hivyo Waziri


ameonyesha kukerwa kwake na kusuasua kwa mkandarasi kumalizia kazi


hiyo kwa muda uliopangwa na kwamba kama asingefuata ushauri wa Katibu


Mkuu wa Wizara ya Maji na Wataalamu wa Wizara yake, basi leo Desemba


6, 2017 ilikuwa siku ya kuvunja mkataba wa Mkandarasi huyo. 

“Hata


hivyo Mkandarasi baada ya kuahidi kukamilisha mradi Februari 8, 2017,


tumeona tumuache hadi muda huo, lakini akishindwa hatuna njia nyingine


ni kuvunja mkataba na kutafuta Mkandarasi mwingine.” Alionya Waziri


Kamwele wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye chanzo cha


maji Mto Wami.


Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete,


amemshukuru Waziri Kamwele na Serikali ya Rais Dkt. John Pombe


Magufuli, kwa nia yake ya dhati ya kuwaondolea kero ya maji wakazi wa


Chalinze, na kwamba ana imani kubwa ya kukamilika kwa mradi huo baada


ya kuulalamikia kwa muda mrefu bungeni kuwa umechelewa sana.


“Mheshimiwa Waziri napenda nikushukuru sana na hasa Mheshimiwa Rais


wetu Mpendwa Dkt. John Magufuli, kwa kazi nzuri ambayo Serikali


inafanya katika kutatua kero za wananchi na hasa wapiga kura wa jimbo


la Chalinze.” Alisema Mhe. Kikwete.
Muonekano wa ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lita milioni 6,
Bagamoyo Mkoani Pwani kama inavyoonekana Desemba 6, 2017
 




No comments:

Post a Comment