Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia
atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano Desemba 27,2017.
Pamoja na mambo mengine Rais Karia atazungumzia miezi minne tokea uongozi
uliopo umeingia madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.
Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na
njia gani inatumika/Itatumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.
Taarifa zaidi za mkutano huo wa Rais Karia na Wahariri,mahali utakapofanyika
pamoja na mualiko utatolewa kwa vyombo vya habari.
Huu ni mkutano wa kwanza wa Rais Karia na Wahariri wa habari za Michezo
tokea ameingia madarakani.
Rais Karia aliingia madarakani August 12, 2017 kwenye uchaguzi
uliofanyika mkoani Dodoma baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi ambao
pia uliwaingiza madarakani Michael Wambura kwenye nafasi ya makamu wa Rais.
Wajumbe wa kamati ya utendaji waliongia madarakani kwenye uchaguzi huo ni
pamoja na
Kanda namba 13 Dar es Salaam
Lameck Nyambaya
Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga
Khalid Abdallah
Kanda No 11 Pwani na Morogoro
Francis Ndulane
Kanda Namba 10 Dodoma na Singida
Mohamed Aden
Kanda Namba 9 Lindi na Mtwara
Dunstan Mkundi
Kanda namba 8 Njombe na Ruvuma
James Mhagama
Kanda namba 7 Mbeya na Iringa
Elias Mwanjala
Kanda Namba 6 Katavi na Rukwa
Kenneth Pesambili
Kanda namba 5 Kigoma na Tabora
Issa Bukuku
Kanda namba 4 Arusha na Manyara
Sarah Chao
Kanda namba 3 Shinyanga, Simiyu
Mbasha Matutu
Kanda namba 2 Mara, Mwanza
Vedastus Lufano
Kanda namba 1 Kagera, Geita
Salum Chama
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF
Desemba 22,2017
No comments:
Post a Comment