Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaji majid Mwanga
kwa kushirikiana na Child Eye and Vision Organization ameanzisha mpango wa matibabu ya macho katika
shule za msingi na Sekondari ili kukabiliana na uono hafifu mashuleni.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti na
muanzilishi wa Child Eye and Vision Organization Dkt. Asha Mweke alisema
wanamshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa kuwatafuta na kuwataka waanzishe mpango wa
kupima macho mashuleni ili kuwaondolea watoto uoni hafifu.
Dkt. Asha alisema wameanza Bagamoyo katika shule
ya Msingi Mbaruku na kwamba mpango huo utakuwa wilaya nzima na baadae mkoa wote
wa Pwani.
Alisema mpango huo wameupeleka mashuleni
kwasababu ndio watoto wengi wana matatizo ya macho na kwamba hakuna mtu
wakuwakagua ili kuwapatia matibabu ya macho.
Nae Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru
Kawambwa ambae ndiyo aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema iko haja
kwa wabunge kuishauri serikali kuanzisha mpango wa matibabu ya macho kwa watoto
kuanzia ngazi ya kaya ili kuwaondolea matatizo ya uoni hafifu.
Alisema watoto wanataraji kusoma ili wapate elimu
ambayo itawasaidia katika maisha yao lakini pia ndio viongozi tunaotarajia kuja
kushika nafasi mbalimbali nchini hivyo wakishindwa kuona darasani hawatafanya
vizuri katika masomo yao.
Alisema tatizo la macho kwa mtoto hawez
kuligundua mapema hivyo hupelekea kushindwa kufahamu vitu vingi kwakuwa
anavyofundishwa darasani.
Alisema endapo Serikali ikianzisha mpango huo wa
matibabu ya macho kwa watoto itasaidia kugundua matatizo ya macho kuanzia
nganzi ya kaya na kulishughulikia tatizo hilo kabla haljawa kubwa
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa
akizungumza na wakati wa kuzindua matibabu ya macho katika shule ya msingi
Mbaruku
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa
akifanya vipimo vya macho wakati wa uzinduzi wa matibabu ya macho mashuleni
wilayani Bagamoyo kushoto ni mwenyekiti wa Child Eye and Vision Organization Dkt. Asha Mweke
Baadhi ya watoto wanaosoma katika shule ya awali
Mbaruku wakiwa kwenye foleni kupima macho yao
Mkurugenzi wa bagamoyokwanza blog ndugu Athumani
Shomari akipata vipimo vya macho wakati wa uzinduzi wa mpango wa kupima macho
kwa watoto wanaosoma shule za msingi na Sekondari Mpango ulioanzishwa na Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo akishirikiana na Child Eye and Vision Organization
Wanafunzi wa shule ya msingi Mbaruku Bagamoyo, wakisubiri
kupimwa macho
Mwenyekiti na mwanzilishi wa Child Eye and Vision Organization Dkt. Asha Mweke akizungumza na waandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment