Sunday, April 23, 2017

SERENGETI BOYS YAPONGEZWA KWA USHINDI.



Serikali imeipongeza Serengeti Boys kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Gabon.

Serengeti Boys wameifunga Gabon katika mechi iliyopigwa nchini Morocco ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika litakalofanyika nchini Gabon.

Msemaji wa Serikali Dk, Hassan Abbas amesema serikali inaipongeza timu hiyo ya vijana chini ya miaka 17 kwa ushindi huo.

Serikali inawasisitiza vijana hao kuendelea kupambana wakiwa wamelenga kufanya vizuri na Watanzania na serikali iko nyuma yao.

Friday, April 14, 2017

YANGA YATOA KAULI POITI 3 ZA SIMBA.

17861429_1877234072550321_8217562871276641628_n
Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi tatu.

Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na mabao matatu ikiwa ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna wanachama wanataka kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku akisisitiza Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka Kombe la Dunia itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”.

“Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la Dunia tena.

”Watu wana hasira zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea. Kagera ni timu ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii kesi.

“Ajabu kabisa, waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si sawa, kuna jambo hapa,” alihoji Mkemi akionekana ni mwenye jazba.

MAUJAJI YA POLISI, RAIS DKT. MAGUFULI ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.

Image result for magufuli images 

MAJAMBAZI YAUA POLISI NANE PWANI.

Image result for IGP Mangu images
Askari polisi  nane wameuwawa na Majambazi mkoani  Pwani.

Tukio hilo  limetokea majira ya  saa 12 na robo jioni  ya  Tarehe 13 Aprili 2017 huko eneo  la Mkengeni kijiji cha  Uchembe kata ya Mjawa Tarafa  ya Kibiti Wilayani Kibiti  Mkoa wa  Pwani.

Ambapo kundi  la majambazi  ambalo idadi yake bado  haijafahamika wakiwa na silaha  walishammbulia kwa risasi Gari la  Polisi lenye namba za usajili PT. 3713  TOYOTA Land Cruiser na kuuwa Askari nane na mwingine mmoja kujeruhiwa mkononi.

Aidha, baada ya  majambazi hao kufanya mauaji walifanikiwa  pia  kuchukua silahatisa kati ya hizo SMG sita zikiwa na risasi 30, kila moja na  Long Range  tatu.

Awali Gari ya  Polisi ilikuwa  ikitokea jarikbu  mpakani kwenye  kizuizi kuelekea Bungu baada ya  kubadilishana zamu ambapo walipofika eneo la Mkengeni  sehemu yenye mteremko na majani marefu walianza Garihiyo ya Polisi ilishambuliwa na  majambazi kwa  kupigwa Risasi kioo cha mbele usawa wa  Dereva na  kusababisha  Dereva kupotezamuelekeo na Gari kuingia kwenye  Mtaro pembenimwa Barabara.

Kufuatia hali hiyo majambazi hao  waliendelea kufyatua Risasi na  kuwauwa Askari Polisi wanane na mwingine  kumjeruhi  mkononi.

KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINT TATU.

IMG-20170413-WA0104-640x427

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 imeipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu kutokana na rufaa waliyoikatia Kagera Sugar kwa kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 2, mwaka huu.

Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba badala ya mchezaji huyo kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizopata mfululizo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku wa April 13, 2017 kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi.

Kwa ushindi huo, Simba sasa inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 26, wakiendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania bara mbele ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 56 wakiwa wamecheza mechi 25.

Ikumbukwe Simba iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kutokana na Kagera Sugar kumchezesha Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 iliyofanyika Aprili 2, 2017 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Katika kikao chake awali Ijumaa iliyopita, Kamati baada ya kupitia malalamiko hayo, iliahirisha shauri hilo hadi leo (April 13, 2017) kujipa muda wa kufuatilia baadhi ya vielelezo kuhusu malalamiko hayo.

“Malalamiko yaliletwa kwetu na timu ya Simba baada ya kufungwa na Kagera Sugar 2-1 kwenye uwanja wa Kaitaba, Simba walileta malalamiko kwamba kuna mchezaji mmoja wa Kagera Sugar Mohamed Fakhi alicheza mchezo huo wakati akiwa na kadi tatu za njano jambo ambalo ni kinyume na taratibu zetu kwa mujibu wa kanuni zetu za ligi,” alisema mwenyekiti wa kamati ya saa 72 wakati akitangaza uamuzi uliofikiwa na kamati yake.

“Tulikaa kikao cha kwanza siku ya tarehe 7 April, 2017 tukajadili, bahati mbaya siku hiyo hatukufanikiwa kufikia mwisho kwa sababu tulikuwa tunakosa baadhi ya taarifa ambazo zinaendana na maamuzi ambayo tungeweza kuyafanya kwa hiyo tulijipa muda hadi leo na tumefanikiwa kuzipata taarifa ambazo tulikuwa tunazitafuta na jioni hii tumefikia maamuzi.”

“Kutokana na nyaraka tulizonazo imethibitika kwamba, mchezaji huyu ambaye anaitwa Mohamed Fakhi alipata kadi ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Mbeya City, akapata kadi nyingine ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Majimaji na pia akapata kadi ya njano kwenye mchezo kati Kagera Sugar na African Lyon.”

“Baada ya kupata malalamiko haya, watu wa Kagera Sugar walikuja juu na kusema kwamba, mchezaji wao alipewa kadi kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na African Lyon na huo ndio utata uliotufanya tutafute ushahidi kuona kwamba hicho kitu kilitokea. Tumepata taarifa na kamati imeridhia kwamba hiki kitu kilitokea na kutokana na hilo, mchezaji huyo alikuwa nje ya sheria 37 (14) na adhabu yake ipo kwenye sheria yetu ambayo inasema kwamba (timu itakayotumia mchezaji ambaye ana kadi tatu za njano, basi itabatilishiwa matokeo na kunyang’anywa ushindi. Timu pinzani itapewa ushindi wa pointi  na magoli matatu).”

Kwa hali hiyo, naomba nitangaze rasmi kwamba, kamati imefikia maamuzi hayo na taratibu zingine zitafuata kuhusiana na hilo.

Tumechukua muda mrefu kutoa maamuzi kwa sababu ya hali ilivyokuwa, kwamba upande wa pili walikuwa wanasema rekodi zao hazioneshi hivyo kwa hiyo ilibidi tutafute rekodi za ziada ndiyo maana tumechukua muda mrefu kutoa maamuzi ya suala hili. Vinginevyo tungetoa maamuzi siku ya tarehe 7 tulipopata malalamiko haya.