Posts

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

Image
  MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza Mamlaka na Taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kujiandaa ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026.   Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo, mara baada ya kupokea taarifa ya utayari na maandalizi ya Serikali kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mvua za El- nino, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam.   Akizungumza na Viongozi pamoja na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zilizochini ya Wizara hizo, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa taasisi zote zinazohusika, kufanya kazi kwa pamoja na kuchukua hatua za tahadhari mapema ili kuzuia au ku...

WAZAZI BAGAMOYO WAPEWA ANGALIZO LA EL-NINO

Image
  Na Omary Mngindo, Lugoba JUMUIA ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imewataka wakazi wilayani humo kuwa makini katika kipindi cha mvua za Elnino zinazotarajiwa kuanza wakati wowote. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Mohamed Mzimba akitoa salamu za Jumuiya kwenye mazishi ya Mke wa Mwenyekiti Mstaafu wa Kijiji cha Mindutulieni Letema Yangalai, yaliyofanyika kijijini humo. "Ukiwa na taarifa ya uwepo wa mvua hiyo unakuwa nwepesi kujua pia kujikinga, ukimuomba Mwenyeezimungu lazima ukalime na sio kukaa chini ya Mti ukisubiri chakula," alisema Mzimba. Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Msoga Debora Rashid aliwataka waTanzania kuendeleza upendo, huku akiwataka wapendane kuanzia kwa jirani na kwamba huo ndio upendo. "Tuangalie sisi wenyewe tupo wapi, tunafanya nini na yele tunayoyasema yanatoka kweli moyoni?  Maana wengi wanajua dhambi ni unzinzi ru, hapana hata kutokumpenda jirani yako na ndugu yako hiyo pia ni dhambi," a...

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 11 SEPTEMBA 2026

Image
 

RC MALISA AAGIZA WATUMISHI KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Image
  RC MALISA AAGIZA WATUMISHI KUTATUA KERO ZA WANANCHI Na Allan Kitwe, Tabora KILA Mtumishi aliyepewa dhamana ya kutumikia wananchi ndani ya serikali hii Mkoani Tabora ametakiwa kuwa mstari wa mbele kusikiliza na kutatua kero zao na sio kusubiri hadi Viongozi wa ngazi za juu wafanye ziara katika eneo lao. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Benno Malisa alipokuwa akiongea na Viongozi mbalimbali wakiwemo watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Wilaya na wengineo juzi. Ameeleza kuwa kila mtumishi yupo kwa ajili ya wananchi hivyo anawajibu wa kusikiliza na kutatua kero yoyote inayomkabili mwananchi au kikundi cha wananchi inayohusiana na idara yake, huu ndio uwajibikaji wa kweli. Amesisitiza kuwa viongozi au watumishi hawakuajiriwa ili wakae Ofisini tu kwenye kompyuta, bali kutembelea maeneo ya wananchi ili kujionea miradi inayotekelezwa, kusikiliza kero zao na kuangalia namna ya kuwasaidia. RC ameagiza Viongozi na Watendaji wa ngazi z...

KAMISHNA WA MAGEREZA MALAWI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA.

Image
  KAMISHNA WA MAGEREZA MALAWI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA. Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi (CP) Tatu Jumbe, Septemba 09, 2026 amepokea ugeni kutoka Magereza nchini Malawi ukiongozwa na Kamishna Milda Salilika ambaye ni Kamishna wa Urekebu na utengamanisho huduma za Magereza Malawi, uliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania mkoani Dodoma kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF Net) unavyofanya kazi. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, CP Tatu Jumbe ameeleza umuhimu wa kubadilishana uzoefu baina ya taasisi za ulinzi na usalama za Tanzania na Malawi, akibainisha kuwa ushirikiano wa aina hiyo unatoa fursa ya kujifunza mifumo bora na kubaini maeneo ambayo yanaweza kuboreshwa kwa manufaa ya askari na taasisi kwa ujumla. Kwa upande wake, Kamishna Milda Salilika kutoka Magereza nchini Malawi, ameeleza namna a...

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU

Image
  KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU Na Albert Kawogo Jumatano 9 Septemba 2026 RAIS wa awamu ya nne , Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika sekta za uzalishaji na usalama wa chakula, teknolojia, uvuvi na uchumi wa buluu. Dkt. Kikwete ameyasema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Sasakawa Peace Foundation ya Japan, Bw. Masanori Kobayashi, katika ofisi yake ndogo iliyopo Masaki, Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalilenga kufuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyoibuliwa wakati wa ziara ya kikazi ambayo Dkt. Kikwete alifanya nchini Japan kuanzia Julai 23 hadi 24, 2025. Katika ziara hiyo, Dkt. Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi sita mashuhuri kutoka Afrika walioalikwa na Serikali ya Japan kupitia taasisi za Sasakawa Peace Foundation na Nippon Foundation. Viongozi hao walishiriki katika kutoa ushauri kuhusu namna bora ya...