RC MALISA AAGIZA WATUMISHI KUTATUA KERO ZA WANANCHI
RC MALISA AAGIZA WATUMISHI KUTATUA KERO ZA WANANCHI Na Allan Kitwe, Tabora KILA Mtumishi aliyepewa dhamana ya kutumikia wananchi ndani ya serikali hii Mkoani Tabora ametakiwa kuwa mstari wa mbele kusikiliza na kutatua kero zao na sio kusubiri hadi Viongozi wa ngazi za juu wafanye ziara katika eneo lao. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Benno Malisa alipokuwa akiongea na Viongozi mbalimbali wakiwemo watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Wilaya na wengineo juzi. Ameeleza kuwa kila mtumishi yupo kwa ajili ya wananchi hivyo anawajibu wa kusikiliza na kutatua kero yoyote inayomkabili mwananchi au kikundi cha wananchi inayohusiana na idara yake, huu ndio uwajibikaji wa kweli. Amesisitiza kuwa viongozi au watumishi hawakuajiriwa ili wakae Ofisini tu kwenye kompyuta, bali kutembelea maeneo ya wananchi ili kujionea miradi inayotekelezwa, kusikiliza kero zao na kuangalia namna ya kuwasaidia. RC ameagiza Viongozi na Watendaji wa ngazi z...