VICTOR
MASANGU, BAGAMOYO
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo amechukizwa na kuona miradi ya maendeleo ipatayo 42
yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1 katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
haijakamilika kwa wakati hadi sasa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya
watumishi na watendaji kufanya kazi kwa mazoea na uzembe hali ambayo
inasababisha hasara kubwa na kukwamisha juhudi za serikali ya awamu ya
tano katika kuwaletea wananchi maendeleo hivyo wote watakaobainika
kuhusika na ubadhilifu wowote wa fedha wachukuliwe hatua kali za kisheria ili
iwe fundisho kwa wengine.
Kauli hiyo aliitoa wakati
wa mkutano maaalumu wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo wenye lengo la kupokea na kujadili majibu ya hoja za
mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa kipindi cha mwaka wa hesabu
kwa mwaka wa 2018/2019.ambapo pia ametoa muda wa siku saba kwa uongozi wa
halmashauri hiyo kufunga hoja zote 38 ambazo bado
hazijakamilika hadi sasa kwani ili kuendana na maagizo yaliyotolewa na serikali
ya Mkoa.
Ndikilo alisema kwamba katika taarifa amabayo
imetolewa na mdhibiti na wa hesabu za erikali CAG imeweza kueleza kuwa kuna
baadhi ya miradi ambayo bado ijakamilika wakati fedha zake zimeshatolewa hivyo
kuna dalili za baadhi ya watendaji kutowajibika kikamilifu katika uetekelezaji
wa majukumu yao.
“Fedha zimetolewa kabisa shilingi
bilioni 1 na milioni 24 lakini mimi nashangaa miradi 42 bado haijakamilika kwa
wakati kabisa hii kwa weli sio sahihi hata kidogo hapa inatakiwa ndugu zangu
madiwani wa baraza hili kuangalia kwa makini maana hii miradi ni mingi kwa hiyo
mimi ninachokiomba miradi hii iweze kukamilika kabisa kwa wakati na kwa wale
watumishi ambao watakuwa wamehusika katika uzembe huu ni lazima wachukuliwa
hatua kali z akisheria.
Aidha Mkuu huyo aliongezea kuwa kwa
sasa inatakiwa hoja zote ambazo ziliitajika kukamilishwa kwa kipindi hiki ni
lazima zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo maana ni agizo ambalo lilishatolewa
na serikali ya Mkoa kwa hiyo mimi naagiza ndani ya siku saba kwa maana ya wiki
moja hoja hizi 38 na kipindi cha mwak 2018/2019 ni lazima zikamilika pamoja na
zile hoja nyingine za miaka iliyopita.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo Zainabu Kawawa amesema licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi kwa
mfululizo kuanzia kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 1019 lakini watendaji na
watumishi wanapaswa kubadilika kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi
hasa katika suala zima la kudhibiti mianya ya upotefu wa mapato pamoja na
kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa katika miradi ya maendeleo.
Kawawa alibainisha kwamba katika
halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo kumekuwepo na changamoto mbali mbali katika
suala zima la ukusanyaji wa mapato hivyo kunahitajika juhudi z amakusudi katika
kuhakikisha mashine ambazo zinatumika katika ukusanyaji wa mapato hayo zinakuwa
zinawashwa kwa lengo la kuweza kuongeza makusanyo tofauti na ilivyokuwa kwa
sasa.
“Hii hali ya ukusanyaji wa mapato
katika halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo sio mzuri ndio ni kweli tumefnikiwa
kupata hati safi kwa awamu nne mfululizo lakini sisi kama viongozi ni lazima
tufuatilie kwa umakini kuhusiana na ukusanyaji w amapato haya mbali mbali
maana nasikia kuna mashine nyingine zinakuwa zimeimwa kwa kipindi cha muda
mrefu sasa hii ni hatari sana lazima mapato yetu yapotee tuu kutokana na uzembe
wa baadhi ya watu,”alisema Kawawa.
Naye mkaguzi wa Ofisi ya Taifa ya
ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali (CAG) wa Mkoa wa Pwani Mwajuma
Kwipunda alibainisha kwamba halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kipindi cha
mwaka 2018/2019 licha ya kuwepo kwa mapungufu ya kutokamilisha mapendekezo kwa
wakati imefanikiwa kupata hati safi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo amefarijika kupokea hati safi kwa mara ya nne mfululizo na
kuahidi kuyafanyia kaiz kwa vitendo maagizo yote nane ambayo yametolewa
na Mkuu wa Mkoa kuhusina na mambo mbali mbali katika kusimamia
utekelezaji wa miradi ya maeneleo pamoja na utekelezaji wa hoja ambazo bado
hazijafanyiwa kazi.
HALMASHAURI ya Wilaya ya
Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani licha ya kupatiwa hati safi mfululuzo kuanzia
kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019 kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa
hesabu za serikali (CAG) lakini bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali
katika masuala ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kutokamilisha kwa baadhi ya
miradi ya maendeleo kwa wakati.
No comments:
Post a Comment