Waendesha
pikipiki wakiwa katika moja ya vituo vyao kazi mjini Bagamoyo.
.........................................
Na
Selestian James.
Waendesha
pikipiki Jimbo la Bagamoyo, wamemshukuru mbunge wa jimbo hilo Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa kwa msaada wa ndoo na sabuni
alioutoa kwao hivi karibuni ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Wakizungumza
na Bagamoyo kwanza blog katika vijiwe mbalimbali vya pikipiki wamesema msaada wa mbunge huyo una
maana kubwa sana kwao kwani tangu awali walitamani sana kuwa na vifaa hivyo ili
kujilinda na ugonjwa huu hatari ambao kwa kiasi kikubwa unasumbua duniani kote.
"Kwa
sasa sisi hatuna budi kumshukuru muheshimiwa mbunge kwani hivi vitu ni muhimu
sana kwetu sisi binafsi, familia zetu na hata wateja wetu kwani kwa sasa
tumejiwekea utaratibu wa kuhakikisha tunanawa kila tunapoingia kijiweni na tumekuwa
tunahakikisha hata abiria zetu wanafanya hivyo pia".
Wamesema
hata abiria pia wanafurahia utaratibu huu kwani wanaona namna tunavyojali afya
zetu na za kwao pia.
"Mwanzoni
tulikuwa tunafikiria sana namna ambayo tungeweza kupata ndoo ukizingatia hivi
vifaa kuna baadhi ya maduka vimepanda bei unakuta ndoo inauzwa mpaka elfu
thelathini, ukizingatia na vipato vyetu vidogo hivyo ilikuwa inatuwia vigumu
sana kuweza kumudu gharama hizo".
Aidha
waendesha pikipiki hao wamemuomba Dkt kawambwa aendelee na moyo huo huo hasa
katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa huo.
"Sisi
tumuombe muheshimiwa mbunge akipata chochote ambacho anachoweza kutusaidia hasa
katika kipindi hiki cha maradhi haya ya Corona basi atufikishie vijana
wake" walisema waendesha boda boda.
Waendesha pikipiki wkiosha mikono yao, katika moja ya vituo vyao kazi mjini Bagamoyo.
Picha zote Na Selestian James.
No comments:
Post a Comment