Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo, 2 Mei 2020 ameshiriki Mapokezi ya Treni ya Kwanza iliyoleta
Makasha 20 kwenye Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Ruvu Kibaha.
Akizungumza kwenye Hafla hiyo Mhe.
Mhandisi Ndikilo amesema Mkoa wa Pwani umejipanga kikamilifu kutumia Fursa za
Kiuchumi na Kijamii zinazotokana na Bandari hiyo.
Amebainisha kuwa Mkoa kupitia
Halmshauri ya Wilaya Kibaha upo katika Mchakato wa kuupanga Mji wa Kwala kuwa
Mamlaka ya Mji Mdogo ili kwenda sambamba na ukuaji wa Shughuli za Kiuchumi
kwenye Eneo hilo.
Aidha ameongeza kuwa Mkoa umeanisha
Ekari 4,000 ambazo zinazunguka Bandari kavu ya Kwala na Mji wa Kwala, Ekari
hizo zitandaliwa Mpango wa Matumizi mbalimbali ikwemo Viwanda Vikubwa, Vidogo,
Maghala, Maegesho ya Magari, Biashara kubwa na Ndogo, Makazi na Makazi
Biashara, Matumizi mchanganyiko kama shule, Mahotel, Hospitali, Nyumba za
Ibada, na shughuli nyingine za Kijamii.
Mhandisi Ndikilo ameeleza kuwa
Mchakato wa kukamilisha matumizi hayo unasimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Akitoa rai ya kuharakishwa kwa
mchakato huo Ndikilo amesema"Shughuli za Bandari kavu zinaanza Lakini
huduma hizi saidizi (Supportive Facilities) Hazijaanza".
Katika hatua nyingine Ndikilo
amewakaribisha Wawekezaji wa viwanda kuja Kwala kuchangamkia Fursa zilizopo
katika Eneo hilo. amesema eneo hilo lipo karibu na Bandari kavu Kwala, lipo
karibu na SGR, lipo karibu na Reli ya TAZARA, lipo karibu na chanzo cha Maji
DAWASA.
"Wananchi wa Pwani na Wawekezaji tutumie Fursa za Kiuchumi na
Kijamii zinazotokana na Bandari hii"
Nae Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye amesema ujenzi wa Mradi huo ni utekelezaji
wa Maagizo ya Mhe. Rais ya kupunguza Msongamano kwenye Bandari ya Dar es
Salaam.
Nditiye amewataka Bodi ya Bandari
kusimamia kikamilifu na kuhakikisha Mradi huu unakamilika kwa asilimia 100
ifikapo Mwezi Juni 2020.
Pia amekubali Ombi la Mhe Mkuu wa
Mkoa wa Pwani la kuwepo kwa Kituo cha Polisi kwenye eneo hilo ili kuimarisha
Ulinzi na Usalama hivyo amewataka TPA kuhakisha kunajengwa Kituo hicho cha
Polisi.
No comments:
Post a Comment