Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC) Dr. James
Matarangio katikati akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 2.036
kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kulia kwake kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa
wananchi wa Mto mkavu ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Gesi asilia (LNG) na kulia
ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano TPDC, Marie Msellemu
...............................................
Na
HADIJA HASSAN, LINDI.
SHIRIKA
la Maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC limekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia
kwa wananchi 693 wa Mtaa wa Likong’o, Masasi ya leo na Mto mkavu ili
kupisha Mradi wa kiwanda cha uchakataji wa Gesi asilia (LNG) katika kata
ya Mbanja Manspaa ya Lindi Mkoani humo kwa kukabidhi mfano wa hundi
ya shilingi bilioni 5.2.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya
Petrol Tanzania TPDC , Dr.James Mataragio kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Godfrey Zambi alisema kuwa kati ya hizo Bilioni 5.2, bilioni 2.3
zitalipwa kwa wananchi wa Mtaa wa Likong’o na Masasi ya leo huku bilioni
2.036 zitalipwa kwa Wananchi wa Mtaa wa Mto mkavu.
Dkt.
Mataragio Alisema mpaka sasa zoezi hilo limekamilika kwa asilimia 88 ambapo
Wananchi wapatao 617 kati ya 693 wameshasaini mikataba ya makubaliano baina yao
na TPDC tayari kwa kulipwa fedha zao huku Wananchi 76 waliosalia wakiwa bado
hawajakamilisha taratibu na nyaraka zao zipo kwenye ukaguzi.
Aidha
Dr, Mataragio aliongeza kuwa zoezi hilo la utowaji wa Mfano wa
hundi linaenda sambamba na ulipaji wa fidia kwa wananchi ambapo mpaka sasa
tayari wananchi mia tatu (300) wa awamu ya kwanza wameshaingiziwa fedha
zao Bank.
Hata
hivyo Dkt. Mataragio alieleza kuwa hatua hiyo ya ulipaji wa fidia ni miongoni
mwa mwendelezo wa hatua za ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa cha uchakataji
wa Gesi asilia (LNG) ambao utagharimu Dolla za kimarekani bilioni 30.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akizungumza mara baada ya
kukabidhiwa mfano huo wa Hundi pamoja na kulipongeza Shirika hilo kwa
kuendesha zoezi la ulipaji wa fidia kwa uwazi pia alitoa onyo kwa
wataalamu pamoja na wananchi wajanja wajanja kuanza kupeleka madai yasiyo
kuwepo.
“kuna
watu watakuja kufungwa hapa kwa sababu ya tamaa , hapa Lindi yupo mtu mmoja
kila madai na migogoro ya Aridhi inapokuja nayeye lazima awepo kila mtaa yeye
yupo tu sasa najiuliza huyo mtu kila mtaa ni wake? Kwa hivyo na hapa napigia
hesabu tukiwaona watu kama hao tutawafunga” alitaadharisha Zambi.
“lakini
pia niwaonye na wataalamu wetu wakati mwingine ipo tabia pia ya kuweka majina
ya watu ambao hawakuwepo, majina hewa. Tusije tukaona majina hewa, na nadhani
tulifanya pia vizuri ya kuhakikisha kwamba kila mtu anakuja hapa
anasimama na anapiga picha mwenyewe” aliongeza Zambi.
Hata
hivyo zambi alitilia mashaka kwa watu 76 ambao hawakujitokeza katika zoezi hilo
huwenda yalikuwa ni majina hewa yaliyotengenezwa na wataalamu wa maeneo hayo
ambao kulingana na uendeshaji wa zoezi lenyewe walishindwa kuwapata.
Mwalimu
kibogoyo ni mmoja ya wa wananchi walioathirika na mradi huo ambapo pamoja na
kukili kuingizia fedha yake ya fidia kwenye Ankaunt yake pia aliliomba shirika
hilo kutoa muda wa kutosha ili wananchi wanaopisha mradi wapate muda wa kutosha
wa kufanya maandalizi mapya ya makaazi yao mapya.
No comments:
Post a Comment