Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa
katika kiwanda cha viuwadudu vya mbu walipofanya ziara katika halmashauri ya
mji Kibaha kwa ajili ya kutembnelea na kugagua miradi mbali mbali ya
maendeleo.(Picha na Victor Masangu)
..........................................
VICTOR
MASANGU, PWANI.
KAMATI ya jumuiya ya umoja wa serikali
za mitaa (ALAT Mkoa wa Pwani imewaagiza watendaji na watumishi wa halmashauri
kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kuweka
mipango madhubuti ambayo itasaidia kusimamia miradi mbali mbali ya
maendeleo ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa bila ya kucheleweshwa kwa
maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti
wa Alat Mkoa wa Pwani Hatibu Chaulembo wakati wa ziara ya kutembelea
miradi mitatu ya kimikakati ikiwemo ujenzi wa machinjio ya kisasa, ujenzi wa
soko, pamoja na kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuulia mazalia ya mbu viuwadudu
ilivyopo katika halmashauri ya Mji Kibaha na kuongeza kuwa wameridhishwa na
hatua ambayo imefikia.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kwamba
serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo inatakiwa isimamiwe ipasavyo na
kukamilika kwa wakati ili kuweza kuwasaidia wanannchi wa maeneo mbali mbali
katika Mkoa wa Pwani waweze kupata fursa za ajira na wengine kujiajiri wao
wenyewe.
“Sisi kama kamati ya Alat Mkoa wa Pwani
tumefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mitatu ya kimikakati katika
halmashauri ya mji Kibaha ikiwemo Soko kubwa la kisasa, ijenzi wa machinjio ya
kisasa pamoja na kujionea shughuli mbalin mbali za uzalishaji amabzo
zinafanyika katika kiwanda cha viuadudu hivyo kwa pamoja tumerudhishwa na
mwenendo mzima japo kuna mambo mengine yanatkiwa yafanyiwe kaza zaidi,”alisema
Chaurembo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Musa Gama ambaye pia ni Katibu wa Alat Mkoa
wa Pwani alimshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kutenga
fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbali mbali ambayo itaweza
kusaidia kwa kiwango kikubwa kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na
kuondokana na wimbi la umasikini.
Gama alibainisha kuwa utekelezaji wa
miradi mbali mbali ya maendeleo ni njia moja wapo ya kuwaondolea wananchi wimbi
la umasikini hivyo juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya awamu tano chini ya
usimamizi mzuri waRais Dk. John Pombe Magufuli hivyo kumamilika kwa miradi hiyo
kutakuwa ni chachu kubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
“Mimi kama Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani
naweza kusema nimejifunz amambo mbali mbali katika ziara hii amabyo tumeifanya
katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwani nimeweza kujionea ujenzi wa machinjio
makubwa ya kisasa pamoja na soko jipya ambayo hivi vyote kwa pamoja vitaweza
kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi pindi vitakapokuja kukamilika kw ahiyo ni
hatua kubwa sana ambayo imefanyika,”alisema Gama.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati YA Alat
Mkoa wa Pwani akiwemo Hamisi Dipakutile, Mshamu Munde pamoja na Jenipher Omolo
alisema kwamba serikali ya awamu ya tano imeweza kufanya mambo mengi katika
sekta mbali mbali hivyo wana imani kuwa katika siku za usoni miradi hiyo pindi
ikikamilika italeta maendeleo makubwa kwa wananchi.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya
jumuiya ya umoja wa serikali za mitaa ALAT Mkoa wa Pwani wakiwa wanapata
maelekezo ya namna ya kutengeneza dawa ambayo inauwa mazalia ya mbu
katika kiwanda cha viuatilifu kilichopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
walipofanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali
za miradi ya maendeleo (Picha na Victor Masangu)
Wajumbe wakiwa katika maabara ya
kuchanagnyia dawa wakifuatilia maelekezo kwa umakini kutoka kwa mtaalamu wa
madawa hayupo pichani walipotembelea kiwanda cha viuadudu vya mbu kilichopo
Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani .(Picha na Victor Masangu)
Mwonekano wa baadhi ya wajumbe wa
kamati ya Alat Mkoa wa Pwani wakiwa katika chumba amabcho kuna mitambo maalumu
ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kuchanganyia madawa ya aina mbali mbali
ikiwemo dawa kwa ajili ya kuulia mazalia ya Mbu.(Picha na Victor Masangu)
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Katibu wa kamati ya Alat Mkoa wa Pwani Musa
Gama akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wataalamu wa kuchanganya madawa
kwa ajili ya kuulia mbu katika kiwanda cha viuadudu walipofanya ziara kwa ajili
ya kujionea shughuli mbali mbali.(Picha na Victor Masangu)
Baadhi wa wajumbe wa kamati ya Alat
Mkoa wa Pwani wakiwa kwa nje ya soko la kisasa ambalo linajengwa Wilayani
Kibaha Mkoa wa Pwani mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo ya kutembelea miradi
mbali mbali ya maendeleo.(Picha na Victor Masangu)
Mmoja w awajumbe wa kamati ya Alat Mkoa
wa Pwani akiwa katika chumba chenye mitambo ambayo inatumika katika
utengenezaji na uzalishaji wa madawa ya kuulia mazalia ya mbu. (Picha na Victor
Masangu)
Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani Musa Gama
kati kati akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya
kumalizika kwa ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika
halmashauri ya Kibaha mji.(Picha na Victor Masangu)
No comments:
Post a Comment