Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wahisani Doris mollel foundation Tika kutoka nchini Uturuki, kwa pamoja wakikabidhi futari kwa wanachi wasiojiweza katika jimbo hilo.
.......................................
Na
SELESTIAN JAMES.
Taasisi
ya Doris mollel foundation kwa kushirikiana na taasisi ya Tika kutoka nchini
Uturuki zimetoa mifuko mia moja na hamsini ya sadaka futari kwa waumini wa dini ya kiislamu
walio katika makundi maalum katika maeneo ya Kiromo kitopeni na hospitali ya
Wilaya Bagamoyo, wilayani Bagamoyo.
Akizungumza
hivi karibuni muwakilishi wa taasisi ya Doris mollel foundation. Doris Mollel
amewashukuru taasisi ya Tika kwa kuwaunga mkono kwa mara nyingine katika
utaratibu wa kugawa futari ambao huwa wanaufanya kila mwaka, katika kusaidia
waislamu hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
shughuli
hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali akiwemo mbunge
wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa na diwani wa kata ya Kiromo Hassan
Usinga, imewawezesha waumini wa dini ya kiislamu katika kata hiyo kupata sadaka
ya futari kwenye mifuko iliyokuwa na maharage, mchele, sukari, chumvi, tambi,
na mafuta.
Kwa
upande wake, muheshimiwa Mbunge Dkt. Kawambwa amezishukuru tasisi hizo kwa
niaba ya wananchi wa Bagamoyo kwa kuona umuhimu wa kutoa sadaka hizo jimboni
humo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo huo wa kuwasaidia watu wasiojiweza
katika mambo mbalimbali na kuwaombea mungu awazidishie kwa kila jema
wanalolifanya.
Amewaomba
waumini hao wa dini ya kiislamu kuziombea taasisi hizo ziweze kufanikiwa katika shughuli
zao za kila siku ili waendelee kutoa faraja kwenye jamii mbalimbali.
Kwa
upande wao wanumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanufaika na msaada huo wa
futari wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Bagamnoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kwa
kuwaletea wafadhili wa kuwa futari.
Wamesema
wao wasingewajua wafadhili hao na kwamba mbunge angeamua kuwapeleka popote
lakini kuwachagua wao watu wasiojiweza ni huruma yake na kuonyesha namna
anavyowajua watu wa jimbo lake.
Aidha,
viongozi na waumini waliokuwepo katika maeneo hayo wamewaombea dua ya
shukurani kuwatakia safari njema na
kuwakaribisha siku nyingine wanapokuwa na sadaka mbalimbali basi wasisite
kufika maeneo hayo.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (wa pili kushoto) akipanga maboksi ambayo ndani yake kuna maharage, mchele, sukari, chumvi, tambi, na mafuta, vilivyotolewa na wahisani Doris mollel foundation naTika kutoka nchini Uturuki.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (kushoto) akiwaweka sawa wananchi wake kwaajili ya kuwapatia msaada wa futari iliyotolewa na wahisani Doris mollel foundation naTika kutoka nchini Uturuki.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (kushoto) akijadiliana na Diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga.
Baadhi
ya walengwa wa msaada wa futari hiyo.
No comments:
Post a Comment