Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa
msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za Michezo nchini,Marehemu
Asha Muhaji ukipelekwa kwenye gari maalum tayari kuelekea kumhifadhi katika
nyumba yake ya milele katika makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar.
......................................
Watu
kadhaa wakiwemo waandishi wa habari wa kada mbalimbali na wanamichezo
wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya aliyekuwa Mwandishi wa habari nguli za
michezo Asha Muhaji (50) ambaye amezikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni
jijini Dar es Salaam.
Katika
mazishi ya marehemu Asha, viongozi wa vilabu mbalimbali na wadau wa soka
wameeleza kuwa kifo chake kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya Michezo na
sekta ya habari hasa za Michezo kwani enzi za uhai wake wake Asha alikuwa
Mwandishi mahiri wa Michezo na alikuwa mfano kwa wengine.
Kabla
ya mwili wake kupelekwa kwenye makaburi hayo kwa ajili ya kupumzishwa, msiba
ulikuwa nyumbani kwao Kijitonyama, Mtaa wa Mabatini jijini Dar s Salaam,
na baada ya mwili wake kuondolewa nyumbani hapo wadau walipata nafasi ya kutoa
salamu zao.
Baadhi
ya waombolezaji waliohudhuria msiba wa Asha Muhaji ni Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia na Katibu wake, Wilfred Kidau,
Msemaji wa Simba SC, Haji Manara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire,
wachezaji na wadau mbalimbali.
Akizungumza
msibani hapo Rais wa TFF Karia amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa
za kifo cha Asha Muhaji na kwamba enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa kwa
TFF katika kuhakikisha nchi yetu inapiga hatua katika soka huku akieleza namna
ambavyo alijitoa kwa timu ya Taifa ya Tanzania ‘ Taifa Stars’
“Tumepoteza
mtu kwenye michezo, ila rai yetu tunayo nafasi ya kuendeleza yale mema ambayo
amefafanua kwa maendeleo ya soka letu.
Wakati
huo huo Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba na Mwalimu wa Soka nchini
Suleiman Matola amesema ni pigo kubwa na kwamba yeye amebahatika kufanya
naye kazi kwa nyakati tofauti hasa kwa kuzingatia kuna wakati alikuwa naye
Simba Simba akiwa Mwalimu na Asha Muhaji akiwa msemaji wa Klabu hiyo.
Msemaji
wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema yeye anafahamu uwezo mkubwa aliokuwa nao
Asha Muhaji enzi za uhai wake katika eneo la uandishi wa habari za michezo na
kwamba mchango wake katika kuhakikisha eneo la michezo linasonga mbele nchini
Tanzania hautasahaulika huku akieleza kuwa Asha alikuwa ni Mwandishi ambaye
muda wowote aliohitajika kufanya kazi yake alikuwa tayari na sio
miongoni mwa waandishi ambao wamekuwa na kasumba ya kuomba fedha kwa
watoa taarifa.
Katibu
Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, kwa upande wake ameeleza namna ambavyo
alikuwa akipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Asha Muhaji na kwamba
ni moja ya waandishi wa habari za Michezo ambaye amejitoa kwa sehemu
kubwa kufanikisha timu ya taifa inafanya vema katika medani ya soka.
Mdau
mwingine wa michezo nchini kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania( JWTZ)
Luteni Suleiman Semunyu amesema kuwa Asha Muhaji enzi za uhai wake
alihakikisha anatumia taaluma yake ya uandishi wa habari za Michezo kuandika
habari za aina mbalimbali za michezo ikiwemo ile ambayo haina umaarufu mkubwa.
Amesema
kuwa Asha Muhaji enzi za uhai wake hakuwa akiandika habari za mpira wa miguu
bali alihakikisha anaandika na habari za Michezo mingine kama Gofu na tenisi.
”Ametangulia
mbele za haki lakini ukweli mchango wake katika medani ya michezo tutaendelea
kuukumbuka, kwetu sisi kila tulipomuhitaji alikuja na pale aliposhindwa alikuwa
anatuletea Mwandishi mwingine, aliaminiwa kwenye kupika waandishi mahiri wa
habari za Michezo.”
Jeneze lenye Mwili wa Marehemu Asha
Muhaji ukiswaliwa nyumbani kwao Kijitonyama,Jijini Dar kabla ya
kumpumzisha kwenye nyumba yake Milele jioni ya leo katika Makaburi ya
Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar es Salaam.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa
msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za Michezo nchini,Marehemu
Asha Muhaji likipakizwa kwenye gari maalum tayari kuelekea kumhifadhi kwenye
nyumba yake ya milele katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watu mbalimbali wakishiriki
mazishi ya aliyekuwa Msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za
Michezo nchini,Asha Muhaji
Rais
wa TFF Wallace Karia (wa pili kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred
Kidau (wa kwanza kulia) wakijadiliana jambo na baadhi ya Wadau wa
Michezo,walipofika kutoka salamu za polenyumbani kwa familia ya Marehemu Asha
Muhaji,ambaye amezikwa leo makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar es salaam.
Msemaji na Mhamasishaji maarufu wa
Simba SC akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Uongozi wa Timu hiyo pamoja na
Wapenzi wa Klabu hiyo nyumbani kwa Marehemu jioni ya leo kabla ya maziko
kufanyika katika makabuli ya Mwinyimkuu Magomeni,Jijini Dar es salaam.
Ndugu,jamaa na Marafiki wakiwa
wamekusanyika nyumbani kwa marehemu Asha Muhaji wakiomboleza jioni ya leo kabla
ya Maziko kufanyika.
Wadau mbalimbali wakishiriki ibada ya
mazishi nyumbani kwa Marehemu Asha Muhaji,maeneo ya Kijitonyama,jijini Dar es
Salaam leo.Marehemu amezikwa jioni ya leo katika makaburi ya
Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar es Salaam.