Saturday, September 30, 2017

NAIBU WAZIRI WA KILIMO AMPA ONYO MUWEKEZAJI CHAURU, WILAYANI BAGAMOYO.

Naibu Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha,mwenye shati la draft akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ruvu, (CHAURU)Sadala Chacha, (kushoto), Kulia mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, majid Mwanga, wakati naibu waziri huyo alipotembelea mashamba ya kilimo cha umwagiliaji cha mpunga Ruvu jana Tarehe 29 Septemba 2017.

Naibu Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha,mwenye shati la draft akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ruvu, (CHAURU)Sadala Chacha, (kushoto), Kushoto kwa Naibu waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, majid Mwanga, na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, wakati Naibu waziri huyo alipotembelea mashamba ya kilimo cha umwagiliaji cha mpunga Ruvu jana Tarehe 29 Septemba 2017.
.......................... 

Naibu Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha, amemtaka muwekezaji wa raia wa China Guo Ming Tang  kuacha kuwakodisha mashamba wanachama wa Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU) ili wanachama hao wafaidike na mashamba hayo ambayo yameandaliwa na Serikali kwaajili ya wananchi.

Kauli hiyo ya naibu waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo, Mifugo na Uvuvi ameitoa  katika mashamba ya ushirika ya Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU) yaliyopo Ruvu katika Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Alisema pamoja na kuacha kuwakodisha mashamba wananchi pia muwekezaji huyo ametakiwa kuacha tabia ya kuwauzia wananchi wanachama wa CHAURU maji kwaajili kumwagilia katika mashamba hayo.

Aidha, alimtaka muwekezaji huyo kufungulia mitaro ya maji yanayoingia mashambani ambayo aliifunga kwa lengo la kuuza maji hayo kwa wakulima na kusema kuwa ni marufuku kuzuia maji hayo ambayo miundombinu yake imetengezwa na serikali kwaajili ya wakulima wa mashamba hayo.

Awali akitoa taarifa mbele ya naibu waziri Mwenyekiti wa Chama cha ushirika Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha alisema wanaiomba wizara kuingilia kati Mgogoro wa muda mrefu baina ya mwekezaji huyo raia wa China na wakulima hali inyopelekea wakulima kukosa haki zao za msingi kama wanachama huku wakitishiwa usalama wao na wengine kupigwa.

Alisema muwekezaji huyo aliingia mkataba kinyume cha sheria mwaka 2012  na mwenyekiti wa CHAURU (wakati huo)  ambapo katika mkatba huo kampuni hiyo ya Guo ming Tang imekabidhiwa ekari 354 za shamba la umwagiliaji lakilimo cha mpunga.


Aidh, pamoja na kukabidhiwa kinyume cha sheria shamba hilo muwekezaji huyo hana uwezo wa kulima shamba lote hilo na badala yake zaidi ya heka 300 anazikodisha kwa wananchi kinyume cha sheria na yeye hulima heka 50 tu.

Akifafanua mazingirz ya mkatba huo Sadala alisema Mkataba huo una mazingirz ya rushwa kwakuwa mkataba huo umetiwa saini na mtu mmoja tu jambo ambalo ni kinyume cha sheria na masharti ya vyama vya ushirika nchini na kwamba mkataba huo haukujadiliwa na Bodi ya CHAURU wala kupitishwa kwenye mkutano mkuu.

Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na kuziba mfereji wa maji unaopeleka maji kwenye  shamba namba 11, kumepelekea ekari 24 kutolimika kwa kipindi cha miaka 5 sasa na kusababisha upotevu wa wastan wa kilo 236,000 za mpunga zenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na laki sita, 200,600,000/=

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ole nasha, amemuagiza Mrajisi wa Mkoa wa Pwani kukaa na muwekezaji huyo ili kupitia upya mkataba huo na kama masharti ya mkataba yamekiukwa hatua za haraka zichukuliwe ili wanachama wa CHAURU wabaki katika mazingira salama ya kufanya shughuli zao za kilimo kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Chama cha Ushirika Ruvu kimeanzishwa mwaka 2002 kikiwa na wanachama 350 wanaofanya shughuli za za kulima mpunga katika eneo la Ruvu na mpaka sasa kuna wanachama 894  ambao wanalima katika shmba hilo lenye ukubwa wa hekta 720.

 Mwenyekiti wa CHAURU Sadala Chacha  alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2015/2016 kimefanikiwa kuzalisha mpunga tani 5.6 kwa kulima hekta 497.4 ambapo msimu wa mwaka 2016/2017. wamefanikiwa kuvuna tani 5.0 kwa kulima hekta 565.6

Sadala alisema katika msimu wa kilimo 2017/2018 wanatarajia kulima hekta 640 na kuvuna tani 7.0  
 Muwekezaji raia wa China, Guo Ming Tang kwenye Mashamba ya Mpunga CHAURU, akisikiliza kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa kilimo, mifugo na Uvuvi.
  Naibu Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Ruvu, (CHAURU) Chacha Sadala, katika eneo la mashamba ya mpunga Ruvu, wilayani Bagamoyo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Ruvu, (CHAURU) Chacha Sadala,akimunesha Naibu waziri miundombinu iliyharibiwa na muwekezaji raia wa China aliyokodishwa ekari 354 katika eneo la mashamba ya mpunga Ruvu, wilayani Bagamoyo, wakati naibu waziri huyo alipotembelea eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, majid Mwanga,(aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mara alipowasili katika ofisi za CHAURU Ruvu

Thursday, September 28, 2017

MAADHIMISHO YA 87 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata keki ya maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho hayo.
Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.