Tuesday, November 7, 2023

TANZANIA, EU KUSHIRIKIANA KUENDELEZA UCHUMI WA BLUU NCHINI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Sera za Uvuvi na Sheria za Masuala ya Bahari kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Bi. Charlina Vitcheva kujadiliana namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kukuza uchumi wa buluu hapa nchini.


Waziri Ulega amekutana na Mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam leo Novemba 7, 2023.


Katika majadiliano yao wamezungumza namna ya kuendelea kufungua fursa za ajira na kukuza uchumi wa jamii hususan wanaoishi katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kwa kuwawezesha zana za kisasa za uvuvi, ufugaji wa Samaki, Kilimo cha Mwani, ufugaji wa majongoo bahari na kaa.


Pia, majadiliano yao yalilenga katika utunzaji endelevu wa mazingira ya bahari wakati wote wa utekelezaji wa miradi ya ukuzaji uchumi wa buluu.


Aidha, Waziri Ulega alimueleza Mkurugenzi huyo kuhusu mradi wa kielelezo wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa BBT- LIFE na kwamba waone namna wanavyoweza kuunga mkono jitihada hizo za kuendeleza vijana kupitia uchumi wa buluu.






No comments:

Post a Comment