Thursday, November 2, 2023

KAMATI YA MAPATO YA HALMASHAURI YAWATAKA WADAU WA BIASHARA KULIPA USHURU KWA WAKATI.

 

Kamati ya mapato ya Halmashauri ya Chalinze ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa mujibu wa mwongozo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri imefanya kikao chake leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi.


Katika kikao hicho Mwenyekiti ameongoza kikao hicho kwa misingi ya kufanya tathmini ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Kamati imefanya tathmini kwa kupokea taarifa ya ukusanyaji mapato kwa vyanzo mbalimbali vya mapato.


Baada ya kikao hicho kamati ya mapato imewaagiza wananchi wote katika Halmashauri ya Chalinze kulipia ushuru na kodi mbalimbali kwa wakati na kuzingatia Sheria taratibu na miongozo ya ulipaji kodi na ushuru huo.


Aidha Kamati hiyo imetoa maelekezo kwa wafanyabiashara kuzingatia taratibu za kufanya biashara kwa kuhakikisha wanakuwa na leseni za biashara na wananchi kuacha ujenzi holela, kujenga pasipo kibali cha Ujenzi ni kosa kwa mujibu wa sheria za mipango miji.


Hata hivyo wajumbe wa Kamati kwa pamoja wamekubaliana kuwa juhudi za ukusanyaji mapato ziongezeke hususan kwa vyanzo ambavyo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha havikufikia asilimia 25 ya makusanyo na kutolewa taarifa ya makusanyo kila wiki.





 

No comments:

Post a Comment