Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega akiteketeza
nyavu haramu zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya
Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 wilayani Chato.
.............................
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega leo ameteketeza zana
haramu katika Ziwa Victoria zikiwemo Nyavu za Makila zilizounganishwa 21710
zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90
pamoja na Pikipiki tano zilizokuwa zikitumia katika kusafirisha Samaki haramu.
Akizungumza na wananchi wa Mwembeni Wilayani Chato Mhe.Ulega amewata
kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kuwafichuwa
haralifu hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini ama
kwenda jela.
”Serikali haitamuonea mtu huruma awe kiongozi au Raia wa kawaida Sheria
itachukuwa mkondo wake nia yetu nikuona Samaki wanaongezaka ziwa Victoria na
watu wavue kwa kufuata sheria ili Taifa liweze kupata mapato pamoja na ajira
kwa wananchi mbalimbali” amesema Mhe.Ulega
Aidha Naibu Waziri huyu amewaonya Wafanyakazi wa Hifadhi ya Rubondo
kuacha tabia ya kupewa rushwana wavivu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu
kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua na kuwapatia
fedha laki mbili hadi tatu.
Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi
haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa victoria ikiwa na lengo la
kuondoa uvuvi haramu pamoja na mitandao ya wafanyabiashara wa zana
haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao
ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
Aidha kiongozi wa oparesheni bwana Gabriel Mageni aliongeza kuwa
katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na tatu baadhi ya mambo
ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa
pamoja na Madiwani wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa
kigeni wanaofanya shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha
hasara Serikali ikiwemo kukosa mapato
mapato.
mapato.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Chato ,Shaban
Ntalambe ,amewataadhalisha
watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu kuwa endapo kuna mtu
hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua kupitia
oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo
awe kiongozi Mkubwa ama mtu wa kawaida.
Mkuu wa Wilaya Chato,Shaban Ntalambe
akishiriki zowezi la akiteketeza nyavu haramu .
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega
akizungumza na wananchi wa Mwembeni pamoja na watumishi na viongozi kuacha
kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla
Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya chato,Shaban Ntalambe
wakielekea katika kisiwa cha hifadhi ya Lubondo.
aibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla
Ulega akizungumza na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Lubondo juu ya kuacha
kushirikiana na wavuvi haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye
hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua.
No comments:
Post a Comment