Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga, akimpatia mtoto dawa ya vitamin A ikiwa ni ishara ya kuzindua chanjo ya vitamin A na dawa za minyoo katika kituo cha Afya Chalinze.
Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga amezindua chanjo ya vitamin A na
dawa za minyoo katika Halmashauri ya Chalinze.
Ktika uzinduzi huo mkuu huyo wa wilaya
amewapongeza watumishi wa Afya katika Halmashauri ya Chalinze ambao wanafanya
kazi kwa kujituma huku akiwataka kuongeza juhudi katika kuwahudumia wananchi.
Aidha, amewataka wale wenye tabia ya kutoa lugha
kali kwa wagonjwa kuacha mara moja na badala yake wazingatie kanuni na taratibu
za kazi yao katika kutekeleza majukumu yao ya kitaalamu.
Majid aliongeza kwa kuwataka wazazi kuwapeleka
watoto wao kupata chanjo ya vitamin A na na dawa za minyoo ili kuwaepusha na
magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika.
wakati huohuo aliwataka kinamama kufika mapema
katika vituo vya Afya na Zahanati kwaajili ya vipimo ili kubaini endapo kuna
tatizo kwa mtoto aliyopo tumboni liweze kushughulikiwa mapema.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mratibu
wa Afya Halmashauri ya Chalinze, Dkt. Miriamu Malekela alisema zoezi
linaloendelea katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kwamba linatarajia
kukamilika Januari 17, 2018
Baadhi ya wazazi waliofika kituo cha Afya
Chalinze kuwapatia watoto wao chanjo ya vitamin A na dawa za minyoo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga
akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Afya Chalinze.
No comments:
Post a Comment