Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, majid mwanga, (kulia) akiwa na askari wa usalama barabarani wakikagua Gari la DANGOTE ambalo limekamatwa kwa kubeba mkaa gunia 78 bila ya kibali ambapo dereva wa gari hilo amekimbia na kuliacha gari kwenye geti laushuru wa mazao ya Misitu Kitongoji cha Sanzale wilayani Bagamoyo.
.......................................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, majid mwanga kwa
kushirikiana na Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS Wilaya ya Bagamoyo
amekamata malori yaliyobeba mazao ya misitu ikiwemo Mkaa, na kuni bila ya kuwa
na kibali.
Akizungumza na waaandishi wa Habari Mkuu huyo wa
wilaya alise magari hayo yaliyokamatwa yanaongozwa na Gari la Mfanyabiashara DANGOTE
ambalo limebeba magunia 78 bila ya kibali kwa lengo la kukwepa ushuru na
kuisababishia serikali mapato.
Gari hilo la DANGOTE lenye namba za usajili T 751
DKA limekamatwa kufuata doria inayofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania TFS wilaya ya Bagamoyo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa uvunaji mazao ya
misitu wilaya ya Bagamoyo ambae ni Mkuu wa wilaya katika kuhakikisha mazao yote
ya misitu yanalipiwa ushuru.
Mkuu wa wilaya Majid mwanga alisema kumekuwa na
tabia ya magari yanayobeba mizigo aina nyingine kujihusisha na ubebaji wa mkaa
kinyume cha sheria huku baadhi ya magari hayo yakiwabandikwa namba za usajili
za bandia.
Aidha, Majid aliwaonya wale wote wanaofanya
biashara za mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu za kukata lessni za uvunaji
na kukwepa kulipa ushuru kuacha mara moja tabia na badala yake wafuate sheria
ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kumpata mmilikiwa gari au mwenye mzigo.
Kwa upande wake meneja wa wakala wa huduma za
misitu nchini wilaya ya Bagamoyo, Joeli Liyangala alisema kuanzia mwezi wa 11
mwaka jana 2017 hadi januari mwaka huu 2018 jumla ya magunia 1436 ya mkaa
yamekamatwa ambayo na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 34 ambapo kati
ya hayo Gari lililobebaba magunia mengi zaidi ni gari la GANGOTE.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akikagua
magari yanayobeba mazao ya misitu bila ya vibali katika eneo Makurunge
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akikagua
magari yanayobeba mazao ya misitu bila ya vibali katika eneo Makurunge, wa pili kulia ni meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Joeli Liyangala.
No comments:
Post a Comment