Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga,
akikagua gwaride kwa wahitimu wa mafunzo ya mgambo (jeshi la akiba) katika
viwanja vya shule ya msngi Vigwaza Halmashauri ya chalinze.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga
amefunga rasmi mafunzo ya mgambo yaliyoendeshwa ndani ya kata mbili za
Makurunge na Vigwaza na kuwataka wawekezaji ndani ya wilaya ya Bagamoyo
kuwatumia kwa shughuli za ulinzi.
Alisema kufuatia viwanda vilivyopo wilayani
Bagamoyo wahitimu hao wa jeshi la akiba wanapswa kupewa ajira ili wafaidike na
fursa zilizopo ndani ya wilaya yao.
Alisema si vyema kuona wawekezaji wenye viwanda
wanachukua walinzi nje ya bagamoyo hali ya kuwa wilaya hiyo imezalisha vijana
wenye uwezo, waaminifu na wenye kujituma katka kazi ya ulinzi.
Aidha, mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo aliwataka
wahitimu hao kuwa waadilifu na kuchunga kiapo cha utii ili watekeleze majukumu
yao kwa mujibu wa sheria.
Akitoa Taarifa ya mafunzo Mshauri wa mgambo
wilaya ya Bagamoyo, Kapteni Matonya alisema ofisi yake inatoa shukrani kwa
ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kuonyesha ushirikiano kuanzia mwanzo hadi mwisho wa
mafunzo hayo.
Alisema mafunzo hayo yamekabiliwa na chnagamoto
mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama za kuchangia michango
mbali mbali inayohusu mafunzo kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Mafunzo hayo ya jeshi la akiba wilayani Bagamoyo
yalianza rasmi Tarehe 01 julai 2017 katika kata za Makurunge na Vigwaza
yalikuwa na wanafunzi 176 ambapo waliofanikiwa kuhitimu ni wanafunzi 144 ambao
kati yao wanaume ni 121 na wanawake ni 23.
Wahitimu wa jeshi la
akiba wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
ambae ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Ahaj, Majid Mwanga.
No comments:
Post a Comment