Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallaah Ulega
ametoa siku 18 kwa Halmashauri ya Bagamoyo kukamilisha zoezi la upigaji chapa
mifugo ili kuondoa usumbufu baina ya wafugaji na jamii ya wananchi wengine.
Kauli hiyo ameitoa mjini Bagamoyo alipokuwa
akizungumza katika kikao kilichowajumuisha wakuu wa idara, viongozi wa uvuvi na
wananchi wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo pamoja na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Bagamoyo, katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo.
Ulega alisema zoezi la upgaji chapa ni agizo la
serikali na kwamba mtumishi yeyote atakaeshindwa kutimiza wajibu wake katika
kutekeleza majukumu yake atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Aidha, aliwaonya maafisa mifugo wanaoshindwa
kutekeleza agizo hilo wakidhani ni swala la kisiasa hatua kali zitachukuliwa
dhidi yao kwa kuaidi amri halali ya serikali ya kutaka Ng'ombe wote kupigwa
chapa.
Alisema zoezi hilo likikamilika litasaidia
kuondoa uvamizi holela wa wafagaji katika maeneo mbalimbali kwakuwa Ng'ombe
wote watafahamika asili ya eneo lao la makazi na hivyo kuondoa kabisa migogoro
ya wafugaji na wakulima inayosababishwa na wafugaji kuhama hama bila ya
utaratibu maalum.
Kufuatia agizo hilo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid
Mwanga ametoa siku mbili kwa maafisa
mifugo wa Halmashauri ya Bagamoyo kuwasilisha mpango wa utekelezaji wa agizo la
kupiga chapa mifugo.
Majid amemuhakikishia naibu waziri kutekeleza
agizo hilo kupitia wataalamu wa idara ya mifugo ndani ya Halmashauri ya
Bagamoyo.
Awali akisoma taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo
na Uvuvi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatuma Latu amesema Halmashauri
ya Bagamoyo ina jumla ya Ng'ombe elfu ishirini na nane mia tano thelasini na
nne 28,534, kati yao Ng'ombe 9,914 tu ndio waliopigwa chapa ambapo sawa na asilimia
34 tu ya ng'ombe wote waliopo ndani ya Halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga
akizungumza na katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo mbele ya Naibu waziri wa mifugo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatuma
Omari Latu akizungumza katika uukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo mbele ya naibu
waziri wa Mifugo na Uvuv, Abdallah Hamisi Ulega.
No comments:
Post a Comment