Muonekano
wa mbele wa Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo
Jaji
Mkuu wa Tanzania,
Prof. Ibrahim Hamisi Juma (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo (kushoto) wakifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa jengo la Mahakama
ya Wilaya ya Bagamoyo ambalo limejengwa Kitongoji cha Ukuni kata ya Dunda.
Jaji
Mkuu wa Tanzania,
Prof. Ibrahim Hamisi Juma (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo (kushoto) wakipeana mikono baada ya kuzindua jengo la Mahakama
ya Wilaya ya Bagamoyo ambalo limejengwa Kitongoji cha Ukuni kata ya Dunda.
Jaji
Mkuu wa Tanzania,
Prof. Ibrahim Hamisi Juma (katikati) akizungumza katika uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo.
............................................
Huduma
za Mahakama katika ngazi mbalimbali hapa nchini bado haziwafikii wananchi zaidi
milioni 25 kutokana na changamoto
mbalimbali ikiwemo upungufu wa majengo ya mahakama.
Hayo
yamebainishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania
Prof. Ibrahim Juma alipokuwa akizindua Mahakama ya wilaya ya Bagamoyo.
Alisema
uboreshaji wa majengo ya Mahakama utasaidia huduma za mahakama kuwafikia
wananchi wengi zaidi na kupunguza changamoto zinazoikabili mahakama za
Taznaznia ikiwemo uchakavu wa majengo.
Alisema
upatikanaji wa haki kwa wakati ndio jambo wanalotarajia wananchi hivyo serikali
inayo wajibu wa kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi na kuzisimamia
katika utekelezaji wake.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, katika kutoa haki kwa wakati ni pamoja na kuzingatia maadili
ambapo wananchi wanataka kuona ngazi zote ili kuwajengea imani na vyombo vyao
vya sheria ikiwemo Mahakama.
Prof.
Ibrahim Juma aliwataka Mahakimu, na wafanyakazi wote katika mahakama ya wilaya
ya Bagamoyo kufanya kazi inayoendana na hadhi ya jengo hilo kwa kutoa huduma bora kwa wakati huku
akiwataka kuepuka kabisa rushwa.
Aidha,
alisema jengo hilo la kisasa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa mahakama
uliozinduliwa rasmi Tarehe 21 Septemba 2016 huko Kibaha Mkoani Pwani na Waziri
Mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Jaji
Mkuu Prof. Ibrahim Juma alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo kwa kuwezesha upatikanaji wa maeneo katika mkoa wake kwaajili ya ujenzi
wa Mahakama.
Alisema
kufuatia juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa wa Pwani, tayari wilaya tatu za mkoa huo
zimepata Mahakama tatu za kisasa ambazo ni Kibaha, Bagamoyo na Mkuranga.
Jaji
Mkuu aliwataka viongozi wengine kwenye mikoa yote na wilaya nchini kutoa nafasi
katika maeneo yao
ili kuona namna ya kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi.
Awali
akizungumza mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo alizitaka mahakama mkoani humo kufanya haraka
kusikiliza na kumaliza kesi ili kuepuka manunung'uniko kutoka kwa wananchi.
Alisema
Mkoa wa Pwani unakabiliwa na migogoro ya wafugaji na wakulima hivyo ni vyema
mahakama zikasimamia haki, usawa na uadilifu katika kutoa hukumu ili aliyekosa
apate adhabu stahiki kulingana na kosa lake na hatimae kila mwananchi aweze kusimama
kwenye utii wa sheria.
Alivitaka
vyombo vinavyosimamia sheria mkoani Pwani kusimamia vyema utoaji wa haki ili
kuepuka kutoa fursa kwa wananchi kujichukulia sheria mikononi.
Mkoa
wa Pwani una jumla ya wilaya 7 ambapo mahakama za wilaya zilizopo ni sita tu na
kufanya upungufu wa mahakama moja ya wilaya.
Aidha,
Wilaya ya Bagamoyo yenye jumla ya kata
26 ina Mahakama za Mwanzo 7 tu ambazo mbili kati ya hizo ndio zenye majengo ya
kisasa huku kata tano zina majengo chakavu na kata 19 zikiwa hazina kabisa
majengo ya mahakama za Mwanzo.
Mahakama
mpya ya wilaya ya Bagamoyo imejengwa Kitongoji cha Ukuni kata ya Dunda ambapo
awali Mahakama ya wilaya ya Bagamoyo ilikuwa jirani na jengo la Halmashauri ya
Bagamoyo.
Kukamilika
kwa Mahakama hiyo ya kisasa ya wilaya ya Bagamoyo kutasaidia katika utunzaji wa
nyaraka ukilinganisha na jengo lile la zamani ambapo kutokana na uchakavu wake
baadhi ya nyaraka zimekuwa zikinyeshewa na mvua au kuliwa na mchwa.
No comments:
Post a Comment