Wednesday, January 10, 2018

VIWANDA BAGAMOYO KUINUA PATO LA WANANCHI.



Mkuu wa Wialaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga (wa pili kulia) akipata maelezo ya mtaalamu na msemaji wa Kampuni ya Euro Plastic LTD, Ally Ornek (kulia kwa mkuu wa wilaya, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hokan PindiEuro Plastic LTD
 ........................................

Ujenzi wa viwanda wilayani Bagamoyo unatarajiwa kuinua pato la wananchi na kuingozea mapato serikali kupitia uzalishaji wa bidhaa ndani ya viwanda hivyo.

Katika ziara ya kutembelea viwanda vilivyojengwa  kata ya Zinga wilayani Bagamoyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Alhaj, Majid Mwanga aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kutoa ajira kwa wakazi wa Bagamoyo ili wananchi wakazi wa Bagamoyo wafaidike na uwepo waa vinda hivyo.

Alisema anafahamu katika kutoa ajira kunazingatia sifa za mwombaji ili kukidhi mahitaji ya kazi inayokusudiwa lakini Bagamoyo waapo vijana wasomi na wenye sifa ambao wanaweza kujituma kwa uzalendo wa Bagamoyo yao na nchi yao kwa ujumla.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya aliwatoa wasiwasi wawekezaji kuhusu tatizo la umeme na kusema kuwa Tayari Shirika la umeme nchini TANESCO wilaya ya Bagamoyo limejipanga kuondoa tatizo la umeme ili kuimarisha uzalishaji wa viwanda hivyo.

Katika kuhakikisha  ujenzi wa viwanda unaimarika wilayani Bagamoy, TANESCO chini ya Wizara ya Nishati inatarajia kupeleka umeme mkubwa chini ya mradi wa North East -3 ambao utaweza kutoa jumla ya 220 KV ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu umeme wa wa eneo la Zinga kufikia mpaka 132 KV.

Aidha, TANESCO wanatarajia kuweka Power plant eneo la Zinga yenye uwezo wa kuzalisha takriban Megawatt 200.

Lakini pia TANESCO ili kuhakikisha umeme huu unakuwa wa uhakika wanatarijia kujenga Bomba la gesi kutoka Tegeta hadi Bagamoyo eneo la Viwanda.

Akizungumzia swala la maji alisema tayari DAWASA wanajenga Tanki kubwa la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita milioni sita ambazo zitasambazwa kwa wakazi wa Bagamoyo pamoja na eneo la viwanda.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo amempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia vyema sera ya viwanda kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Akizungumzia fursa za ajira msemaji wa Kampuni ya Euro Plastic LTD, kuoka nchini Uturuki, ALLY Ornek alsema katika viwanda wanavyotarajia kujenga vinaweza kuajiri wafanayakazi zaidi ya elfu tano.

Alli aliongeza kuwa zaidi ya vitano vianatarajiwa kujengwa vikiwemo viwanda vya kutengeneza bomba za Plastic, Vipodozi, na Kiwanda kikubwa cha Nondo.

Miongoni mwa viwanda ambavyo Mkuu wa wilaya aliweza kutembelea kata ya Zinga, ni pamoja na kiwanda cha African Dragon ltd, ambacho kinachakata mabati kabla kuwekwa migongo, kiwanda cha Phiss Turney ambacho ni cha kuchakata ngozi, kiwa cha Eco Consumer Product kinachotengeneza vipodozi pamoja na vifungashio vya bidhaa vikiwemo kopo na chupa za bidhaa mbalimbali.

Aidha, kiwanda kingine ni kile kinachotengeza chakula cha mifugo mbalimbali. 


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa kiwanda cha Euro Plastic LTD pamoja na wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Bagamoyo alipofanya ziara ya kutembelea viwanda vilivyopo kata ya Zinga wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiangaia bidhaa ya mafuta inayozalishwa na kiwanda cha Eco Consumer Product kilichopo Zinga wilayani Bgamoyo, kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Mhandisi Albert Lema.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, akiweka lebo kwenye chupa ya mafuta yanayozalishwa na kiwanda cha Eco Consumer Product wakati alipotembelea kiwandani hapo kujionea shughuli za uzalishaji.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,( wa pili kulia) akiangalia bati ambalo linaandaliwa katika kiwanda cha Arfan Dragon LTD.





No comments:

Post a Comment