Posts

RAIS SAMIA AMJULIA HALI MAMA FATMA KARUME.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Mama Fatma Karume, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba, Zanzibar, tarehe 11 Agosti, 2026.

DIWANI WA KEREGE BAGAMOYO, AFIKISHA KILIO CHA WANANCHI DAWASA.

Image
  Na Mwandishi wetu, Bagamoyo. Mhe. Diwani wa kata Kerege ndugu Yusuph Ngoroge Augost tarehe 10, 2026 alifanikiwa kufika ofisi za Dawasa Mapinga kujadiliana na Meneja wa Dawasa tawi la Mapinga kuhusu changamoto ya maji ya vitongoji vya Kitonga, Nyakahamba na Kilemela. Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi mara baada ya kutoka ofisi za DAWASA Mapinga, Diwani huyo wa kata ya Kerege, Mhe. Ngoroge, amesema Kitongoji cha Kitonga kimekuwa na changamoto ya maji kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ambapo maji hayatoki kwa wakati. Alisema Kitongoji cha Kitonga ndio kuna kituo cha Afya ambapo matumizi ya maji ni makubwa kulingana na umuhimu wake. Mh. Diwani alifikisha kilio hicho kwa niaba ya wananchi wake ambao wamekuwa wakikosa maji kwa muda mrefu hali inayoleta usumbufu kwa wananchi wa vitongoji hivyo. Meneja alipokea changamoto na kukubaliana na Mhe. Diwani kuwa siku ya Ijumaa Augost 14, 2026  watatembelea maeneo yote ili kuona jinsi ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo. Meneja huyo wa ...

DKT. NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR, NI MGENI RASMI UZINDUZI WA JENGO LA DAKHALIA SKULI YA HUSNUU MAKAME

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Zanzibar, leo tarehe 11 Agosti 2026.  Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Jengo la Dakhalia katika Skuli ya Sekondari ya Husnuu Makame – Kibuteni Unguja, ikiwa ni shamrashamra ya Tamasha la Kizimkazi. (Kizimkazi Festival 2026)

RAIS. DKT. MWINYI AKUTANA NA MKURUGENZI WA TDB

Image
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ally Mwinyi,  amekutana na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Trade and Development Bank (TDB), Bw. Admassu Tadesse, pamoja na ujumbe wake, kwa mazungumzo kuhusu fursa za kupata vyanzo vipya na vyenye unafuu vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati Zanzibar. Ameeleza umuhimu wa kuangalia mifumo mbalimbali ya kifedha inayoweza kuendana na mahitaji yetu ya maendeleo, ikiwemo katika Bandari Jumuishi ya Mangapwani, nishati, mafuta na gesi, tafiti yakinifu pamoja na kuimarisha taasisi za fedha za ndani. Aidha, amezungumzia umuhimu wa kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia vyanzo vya nishati mbadala, pamoja na kupanua uwekezaji katika sekta ya makaazi, ikiwemo pendekezo la ujenzi wa nyumba 10,000 kupitia Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC). Ameeleza pia utayari wa Zanzibar kuangalia fursa za kupata wawekezaji kupitia mtandao wa TDB katika miradi yenye tija na umuhimu wa kimkakati.  TDB imemuhakikishia D...

MATUMIZI YA INTERNET NCHINI YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 6.4 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MITATTU.

Image
  Matumizi ya huduma za intaneti yamezidi kuongezeka kutoka milioni 58.9 mwezi Machi 2026 hadi kufikia milioni 62.7 mwezi Juni 2026, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 6.4. Kwa mujibu wa ripoti ya Hali ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka iliyoishia Juni 2026, inaonesha idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma ya Intaneti angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bila kujali teknolojia iliyotumika. Ripoti hiyo imefafanua kuwa huduma ya intaneti kwa njia ya simu za mkononi inapendelewa zaidi ikiwa na jumla ya laini milioni 37.6 ikilinganishwa na huduma ya intaneti isiyohamishika. Kuongezeka kwa utumiaji wa intaneti kunatokana na ubora wa huduma na miundombinu inayowezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa kidijiti.

RAIS DKT. SAMIA ATEMBELEA MJI MKONGWE ZANZIBAR

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mfano wa Mlango wa Zanzibar (Zanzibar door) baada ya kuwasalimia wazee wa Mji Mkongwe (Stone Town), Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mfano wa Jahazi wakati alipowatembelea Wananchi wa Jaws Corner katikati ya Mji Mkongwe, Zanzibar tarehe 10 Agosti, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akicheza mchezo wa bao baada ya kuwasalimia wananchi wa Mji Mkongwe (Stone Town) katika eneo la Jaws Corner, Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza nyimbo mbalimbali za Taarabu asilia baada ya kuwasili katika eneo la Jaws Corner katikati ya Mji Mkongwe (Stone Town), Zanzibar tarehe 10 Agosti, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na vijana wa Makachu pemb...

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMANNE TAREHE 11 AGOSTI 2026

Image