Posts

UMARUKI WATUMIA MILIONI 7, KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO PWANI.

Image
  Viongozi wa Umoja wa Maendeleo wa Watu wa Rufiji mkoani Pwani na Kilwa mkoani Lindi (UMARUKI) waishio Morogoro, wakikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani ambao umepokelewa na Katibu tawala mkoani Pwani (RAS)  Rashid Mchata kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo. .................................... Na Rashid Mtagaluka, Kibaha. Umoja wa Maendeleo wa Watu wa Rufiji mkoani Pwani na Kilwa mkoani Lindi (UMARUKI) waishio Morogoro, jana Mei 23/2024 umekabidhi msaada wa nguo kwa wananchi waliopatwa na athari ya mafuriko mkoani Pwani. Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa wa Pwani, Katibu Mkuu wa UMARUKI Bwana Juma Mtumbei alisema umoja huo umeguswa na tukio hilo, hivyo kama binadamu wameona wanao wajibu wa kuwasaidia. Kwa mujibu wa Mtumbei, msaada waliotoa kwa waathirika hao ni pamoja na nguo za watoto, wanawake, wanaume pamoja na nguo maalumu za kujistiri wakati wa baridi zote zikiwa na  thamani ya shilingi Milioni Saba na laki saba. Kwa upan...

MAJALIWA: TUMEDHAMIRIA KUONGEZA KIPATO CHA WANANCHI

Image
  Asema lengo ni kuleta uwiano mzuri wa kiuchumi na kijamii mijini na vijijini WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya imedhamiria kuongeza ushiriki wa wananchi katika kujenga uchumi wa viwanda, kuongeza kipato kwa wananchi wengi na kuleta uwiano mzuri wa kiuchumi na kijamii mijini na vijijini. “Ili kufikia lengo hilo, Serikali inatekeleza Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini kwa kufanya mapitio na maboresho ya sera, sheria na kanuni ambazo zinakuwa ni kikwazo katika ufanyaji wa biashara nchini.” Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 23, 2024) kwenye ufunguzi wa Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji baina ya Uganda na Tanzania, katika Hoteli ya Johari Rotana jijini, Dar-es-Salaam. Amesema Serikali imeimarisha utoaji huduma kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki 55 ya taasisi 50, pia sheria 13 zimeshafanyiwa marekebisho ili kupunguza au kuondoa kodi, ada na tozo na kupunguza au kuweka misamaha ya ushuru wa forodha. “M...

JKT RUVU WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA SEKTA YA UTALII.

Image
  Kanali Peter Mnyani (Mwenye suti) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John wakifunua kitambaa kuashiria kuzinduliwa kwa zuu hiyo. Picha na Omary Mngindo. .................................... Na Omary Mngindo, Ruvu. JESHI kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, imeunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Saluhu katika suala la kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo vikiwemo vya wanyamapori kupitia sekta ya utalii. Hatua hiyo inatokana na kambi ya Ruvu kuanzisha kitalu cha kuhifadhia wanyama hao, kwa kutenga ardhi yenye ukubwa wa eka 70, pembezoni mwa kambi wakianza na Twiga, Swala, Pundamilia na wengine wadogowadogo. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kikosi hicho Kanali Peter Mnyani, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John, wakati wa uzinduzi wa zuu hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanajeshi wastaafu na mamia ya wananchi. "Mkuu wa Wilaya uanzishwaji wa zuu ya wanyama tunalenga kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu, ambae ...

BENKI YA NBC YAZINDUA BIMA YA AFYA KWA WAKULIMA

Image
  YATAMBULISHA KAMPENI YA KUHAMASISHA KILIMO CHA UFUTA LINDI NA MTWARA Na Hadija Omary  LINDI Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Assemble Insurance imezindua huduma ya Bima ya Afya kwa wakulima nchi nzima ikilenga kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa kundi hilo. Hatua hiyo inatajwa kuwa itasaidia kuimarisha sekta ya afya ambayo ni moja ya nguzo muhimu katika ukuaji wa kilimo nchini. Kupitia huduma hiyo wakulima na familia zao wanaweza kupata huduma ya bima ya afya kwa malipo ya kiasi cha Sh. 450,000 kwa mwaka. Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo imefanyika leo mkoani Lindi ikienda sambamba  na uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la ufuta mkoani Lindi na wilaya za Masasi na Nanyumbu mkoa wa Mtwara. Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi Zuwena Omary aliongoza hafla hiyo iliyohusisha viongozi wa vyama vya msingi na ushirika mkoani Lindi na Mtwara huku Mku...

WAZAZI NA WALEZI MKOANI LINDI WATAKIWA KUTUMIA MIFUMO RASMI KATIKA KUMALIZA MIGOGORO YAO

Image
  NA HADIJA OMARY LINDI. Wazazi na walezi Mkoani Lindi wametakiwa kuitumia vyema mifumo iliyowekwa na Serikali katika kushughulikia migogoro na tofauti zinazojitokeza katika familia zao  ambayo kwa kiasi kikubwa huchangia kuachana na  kusababisha watoto kuathiriwa kwa kukosa  malezi imara. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo  katika maadhimisho ya siku ya Familia ambayo kwa ngazi ya Mkoa yamefanyika katika viwanja vya soko la majengo halmashauri ya Mtama Mkoani humo. Ndemanga amesema  Mifumo hiyo ni pamoja na madawati ya jinsia na Ofisi  za ustawi wa jamii zilizopo kwenye kila halmashauri. Ndemanga ametaka wazazi kuitumia siku hiyo kutafakari namna ya kuimarisha ubora wa familia ikiwemo kutafuta suluhu ya tofauti zao kwa njia zinazofaa ili zisiendee kuathiri malezi na makuzi ya watoto. “Watoto wetu wakati wanaimba wamekuambia kwa lugha nyepesi sana kwamba tunapogombana baba anakuwa na lakwak...

BUWASA IPO TAYARI KUSAIDIA KPC

Image
  Na Alodia Babara, Bukoba Mwakilishi wa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba BUWASA mhandisi Matage Doto amesema mamlaka hiyo iko tayari kushirikiana na wadau wengine kusaidia  chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kagera (KPC) katika ujenzi wa ofisi ya chama hicho. Hayo yamekuja baada ya mwenyekiti wa club ya waandishi wa habari mkoani hapa Mbeki Mbeki, kumuomba mgeni rasmi kutoa msaada katika ujenzi wa ofisi ya waandishi wa habari kutokana na club hiyo kuwa na kiwanja ambacho tayari kimeishapata hati miliki. Mhandisi Doto wakati akihutubia waandishi hao Mei 15,2024 wakati akiwa mgeni rasmi kwa niamba ya Mkurugenzi wa BUWASA katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika kimkoa mjini Bukoba ametoa pongezi kwa club hiyo kwa mawazo ya ujenzi wa ofisi na kusema kuwa, endapo club hiyo itaanza ujenzi ishirikishe wadau mbalimbali ikiwemo mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba (BUWASA.) “Niwapongeze kwa kuwa na mawazo ya kuwa na...

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 40 MTAMA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA

Image
  Na HADIJA OMARY  LINDI. Zaidi ya wananchi Elfu 40 kutoka katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wanatarajiwa kunufaika na mradi wa Maji na usafi wa mazingira unaotekelezwa  na taasisi isiyo ya kiserikali ya 'Heart to Heart' chini ya ufadhili wa Shirika la Kimataifa la KOICA utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo katibu tawala Mkoa wa Lindi Bi zuwena Omary amewahimiza wananchi na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa huo kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili viendelee kutoa maji kwa muda mrefu.  amesema upatikanaji wa maji safi na ya uhakika unategemea na utunzaji wa mazingira kuzunguka vyanzo vya maji  ikiwemo upandaji miti huku pia akitaka kamati za maji na mazingira zishirikishwe ili kufikia malengo ya mradi huo. Mratibu wa mradi kutoka Heart to Heart Innocent Deus  amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa miaka sita kwa awamu tofauti ambapo kwa awamu ya kwanza utatekelezwa kwa miaka mitatu katika ...

WASITISHA MASOMO BAADA YA SHULE YAO KUGEUKA MAKAZI YA WANANCHI WAATHIRIKA WA KIMBUNGA HIDAYA.

Image
  Na Mwandishi wetu Lindi Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha tarehe 04 Mei 2024   kama ilivyotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa saa 36 mfululizo ilisababisha  maafa makubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi huku wengi wao waliofikwa na maafa hayo wakijikuta wamekosa makazi, malazi na hata chakula.   Kijiji cha Mchakama kilichopo Wilayani Kilwa ni miongoni mwa  maeneo yaliyokumbwa na athari hizo za mafuriko ambapo zaidi ya kaya 400 zimekosa makazi huku wananchi1000 wakilazimika kuishi katika vyumba vya Madarasa vya Shule ya msingi Mchakama.   Hali hiyo ya vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Mchakama kutumika kama makazi kwa wananchi hao imesababisha wanafunzi zaidi ya 200 wanaosoma shuleni hapo kulazimika kukatisha masomo yao.     Mohamedi Mwadini ambae ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mchakama alisema shule hiyo inajumla ya Wanafunzi 291 ambao kati yao  138 ni wasichana na...

MANISPAA YA LINDI YAINGIA MAKUBALIANO YA BIASHARA YA HEWA UKAA

Image
  NA HADIJA OMARY  LINDI. Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Lindi  limepitisha mkataba wa makubaliano ya Biashara ya hewa ukaa katika vijiji 10 , jumuhiya za uhifadhi wa Misitu 3  na msitu wa hifadhi wa manispaa na kampuni ya village climate solution limited (VCSL). Wakizungumza katika kikao cha robo ya tatu ya baraza hilo ,  madiwani  hao wamesema kuwepo kwa biashara hiyo kutaiongezea Halmashauri chanzo kipya cha mapato na kwamba mradi huo utakuwa na manufaa kwa Manispaa na wananchi kwa ujumla Meneja wa Mradi huo  yahya Mtonda amesema Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi kisichopungua miaka 40 katika Vijiji   vya Kiwawa, Mputwa, Milolo magharibi, Ruhoma, Muungano, Kinyope, Likwaya, na Makumba. " sambamba na vijiji hivi mkatamba huu umehusisha jumuhiya za uhifadhi wa Misitu ambazo zimeanzishwa pembezoni mwa Mtaa wa Nandambi, pamoja na msitu wa hifadhi wa Makangara katika Manispaa hii ya Lindi nao pia umeingia katika Biashara ya...

JUMUIYA YA WAZAZI BAGAMOYO YASIMAMISHA UPIMAJI ARDHI CHALINZE.

Image
  Na Omary Mngindo, Chalinze. JUMUIA ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imeitaka Idara ya Ardhi halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani hapa kusitisha upimaji wa ardhi katika eneo linalomilikiwa na Jumuia hiyo. Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Aboubakary Mlawa, katika kikao kilichojumuisha wanachama wa Jumuia kwenye kuelekea sherehe za Wazazi Kitaifa, itayotanguliwa na ya Mkoa ambapo kiwilaya imefanyika Kata ya Bwilingu. Alisema kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa  ekari 50, Jumuiya hiyo ilipewa na uongozi wa Kijiji mwaka 2000 kwaajili ya kujenga shule ya wazazi, lakini wavamizi wametoa alama za mipaka ya eneo hilo na kujenga na sasa wanarasimisha  rasmi ili wapatiwe hati. "Ardhi ni yetu hivyo kuwabana wale ambao wameingia watalazimika kutulipa hela yetu kulingana na thamani ya ardhi ya sasa, hatutawanyang'anya ila watafidia maeneo yetu kulingana na thamani ya sasa," alisema Mlawa. Aliongeza kwamba "Mimi msimammo wangu ni huo zoez...