Posts

Waziri wa nishati ataka wawekezaji kuzalisha vifaa vya kusafirisha gesi hapa nchini

Image
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa wito kwa wadau wa viwanda kutengeneza Vifaa vya kusafirisha nishati ya mafuta na gesi hapa nchini dhamira ikiwa ni kuharakisha mchako wa kuanza miradi ya usambazaji lakini pia kupunguza gharama za uzalshaji. Alisema uhitaji wa mabomba kwa miradi inayoendelea bado ni mkubwa na kwamba hadi sasa mahitaji ya mabomba ya gesi ni kilometa  zisizopungua 2,250 na mita za luku ni 8,000 hadi 10,000 kwa mwaka . Aidha akizungumzia kasi ya usambazaji wa mabomba ya gesi majumbani, Kalemani alisema kuna mafanikio makubwa yamepatikana ikiwamo usambazaji huo kuongezeka kutoka Kaya 70 hadi kufikia Kaya 1000 kwa Miaka mitatu. Aliongeza kusema kuwa kuagiza vifaa nje ya nchi kunapoteza mapato ya nchi, agizo alilolitoa linalenga kulinda mapato, uzalishaji wa mabomba koki ,vyuma, nyaya utasaidia  kujenga uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda ,"Dkt.Kalemani . Faida ya kuzalisha mabomba nchini itasaidia kuongezeka kwa kasi ya kusambaza gesi na hivyo kuwap...

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Ateta Na Madereva Wa Malori, Namanga

Image
  Arusha. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba. Dkt. Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona. Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga. “Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa ” alisema. Aidha, Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwa...

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KARIBUNI

Image
Na Iisac Thadeo   Kampuni inayosimamia mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki  (EACOP)imefanya kikao na waziri wa Nishati nchini Tanzania Dr.Medard Kalemani kwa lengo la kuitaarifu Serikali maendeleo ya mradi katika eneo la Ziwa Albert nchini Uganda pamoja na maendeleo ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki  (EACOP) Vilevile kampuni ya Total na wizara ya Nishati wamezungumzia mipango ya kuendelea na mazungumzo ya makubaliano ya Serikali husika (wenyeji)wa makubaliano ya wabia /wanahisa,pamoja na makubaliano ya maswala ya Usafirishaji ili kuleta uiano wa makubaliano yote kwa ajili ya kuendelea na maamuzi ya mwisho ya uwekezaji Kwa upande wake waziri WA Nishati wa Tanzania na kwa niaba ya Serikali ya Tanzania amesema leo ni siku nzuri kwa wenzetu wa Total wametuarifu wamekamilisha majadiliano Kati Yao na Sino kutoka Uingereza na Total wamechukua his a asilimia 67 na nyingine zilizobaki za SINO kwa maana hiyo atakuwa ni mwekezaji mkubwa. Aidha wazi...

KAMATI YA ALAT PWANI YAIFAGILIA MIRADI YA UJENZI WA SOKO NA MACHINJIO KIBAHA MJI.

Image
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika kiwanda cha viuwadudu vya mbu walipofanya ziara katika halmashauri ya mji Kibaha kwa ajili ya kutembnelea na kugagua miradi mbali mbali ya maendeleo.(Picha na Victor Masangu)  .......................................... VICTOR MASANGU, PWANI.   KAMATI ya jumuiya ya umoja wa serikali za mitaa (ALAT Mkoa wa Pwani imewaagiza watendaji na watumishi wa halmashauri kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa  kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia  kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa bila ya kucheleweshwa kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Hayo yalibainishwa  na Mwenyekiti wa Alat Mkoa wa Pwani  Hatibu Chaulembo wakati wa ziara ya kutembelea miradi mitatu ya kimikakati ikiwemo ujenzi wa machinjio ya kisasa, ujenzi wa soko, pamoja na kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuulia mazalia ya mbu  viuwadudu ilivyopo ka...