Wednesday, June 10, 2020

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KARIBUNI




Na Iisac Thadeo

 Kampuni inayosimamia mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki  (EACOP)imefanya kikao na waziri wa Nishati nchini Tanzania Dr.Medard Kalemani kwa lengo la kuitaarifu Serikali maendeleo ya mradi katika eneo la Ziwa Albert nchini Uganda pamoja na maendeleo ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki  (EACOP)

Vilevile kampuni ya Total na wizara ya Nishati wamezungumzia mipango ya kuendelea na mazungumzo ya makubaliano ya Serikali husika (wenyeji)wa makubaliano ya wabia /wanahisa,pamoja na makubaliano ya maswala ya Usafirishaji ili kuleta uiano wa makubaliano yote kwa ajili ya kuendelea na maamuzi ya mwisho ya uwekezaji

Kwa upande wake waziri WA Nishati wa Tanzania na kwa niaba ya Serikali ya Tanzania amesema leo ni siku nzuri kwa wenzetu wa Total wametuarifu wamekamilisha majadiliano Kati Yao na Sino kutoka Uingereza na Total wamechukua his a asilimia 67 na nyingine zilizobaki za SINO kwa maana hiyo atakuwa ni mwekezaji mkubwa.

Aidha waziri Kalemani alisema amewaomba Total na kuwataka yote wanayosema wayafanye kwa haraka

Mkutano huo ulifanyika zilipo Ofisi ndogo za wizara ya Nishati jijini Dar es salaam na kuudhuliwa na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo kuwepo Katibu mkuu wa wizara hiyo mheshimiwa Zena

No comments:

Post a Comment