Wednesday, June 10, 2020

Waziri wa nishati ataka wawekezaji kuzalisha vifaa vya kusafirisha gesi hapa nchini





Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa wito kwa wadau wa viwanda kutengeneza Vifaa vya kusafirisha nishati ya mafuta na gesi hapa nchini dhamira ikiwa ni kuharakisha mchako wa kuanza miradi ya usambazaji lakini pia kupunguza gharama za uzalshaji.

Alisema uhitaji wa mabomba kwa miradi inayoendelea bado ni mkubwa na kwamba hadi sasa mahitaji ya mabomba ya gesi ni kilometa  zisizopungua 2,250 na mita za luku ni 8,000 hadi 10,000 kwa mwaka .

Aidha akizungumzia kasi ya usambazaji wa mabomba ya gesi majumbani, Kalemani alisema kuna mafanikio makubwa yamepatikana ikiwamo usambazaji huo kuongezeka kutoka Kaya 70 hadi kufikia Kaya 1000 kwa Miaka mitatu.

Aliongeza kusema kuwa kuagiza vifaa nje ya nchi kunapoteza mapato ya nchi, agizo alilolitoa linalenga kulinda mapato, uzalishaji wa mabomba koki ,vyuma, nyaya utasaidia  kujenga uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda ,"Dkt.Kalemani .

Faida ya kuzalisha mabomba nchini itasaidia kuongezeka kwa kasi ya kusambaza gesi na hivyo kuwapa nishati wananchi kwa wakati.

Naye Naibu Waziri wa  Wizara hiyo Stephen Byabato   amesema serikali inaendelea kutekeleza ilani ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuendelea kuwaunganisha nishati ya umeme mjini na vijijini.

Alisema Rais Dkt.Magufuli anaamini vijana wana uwezo kiutendaji ndio maana amemteua kumsaidia kutekeleza majukumu ya Wizara hiyo chini ya Waziri Dkt.Kalemani.

Awali akizungumza kwenye Mkutano huo, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo la Petroli TPDC Dkt. James Mataragio amesema wanaendelea na ujenzi wa vituo vitano vya kujaza gesi asilia kwenye magari katika mkoa wa dar es salaam huku kukiwa na mpango wa kupeleka nishati hiyo jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment