Sunday, November 18, 2018

MWENYEKITI UWT PWANI AMPONGEZA RAIS MAGUFULI.

MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Farida  Mgomi amempongeza mwenyekiti  wa ccm taifa  ambaye pia ni Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa viteendo vyake anavyovifanya nchini kwa kuwajali watu  wanyonge ambao ndio wapiga kura wa chama tawala.

Alisema hayo alipokuwa akizungunza ktk kikao cha kawaida  kuhusu kutumia fursa zinazotolewa na serikali  kwa lengo  la kuwakomboa wanawake wa Tanzania kiuchumi.

Mgomi alisema  kuwa  kipindi  hiki  si cha  kujiweka  nyuma nyuma kwani serikali ya awamu  ya tano imeziagiza Halmashauri kote nchini kuhakikisha zinawapatia kina mama mikopo isiyokuwa  na riba.

"Rais  Dkt John Pombe Magufuli amekuwa kimbilio la watu wa chini  hii  ni kutokana na umahiri wa ccm ktk utekelezaji wake wa ilani" Alisema Mgomi. 

Aidha  mwenyekiti huyo  amempomgeza Rais Dkt John Pombe  Magufuli kwa kitendo chake  alichokifanya kwa  wakulima wa korosho  kwani ameongeza thamani zaidi ya Chama Cha Mapinduzi kwa wakulima kuwa hakuna mkukima wa kuteseka kipindi cha serikali ya awamu ya tano.

"Uchaguzi ujao kama vile tunasukuma mlevi tu kwani ahadi zote  zilizokuwa zimesemwa wakaati tunajinadi tumezitekeleza kwa asilimia 90% hivyo  lazima  ccm tushinde  kwa kishindo " Aliongeza Mwenyekiti wa Uwt mkoa wa pwani.

Kwa upande  wake Apsa Juma  amempomgeza Mwenyekiti huyo wa UWT kwa kitendo chake cha kuwakutanisha wanawake wa mlandizi na  kuwafumbua macho juu ya kutokuogopa kukopa fedha kwa ajili ya kufanya maendeleo.

Aliongeza  kuwa kipindi hiki kimekuwa tofauti kwani kila  kitu  kiko wazi .

WAKULIMA WA KOROSHO WA KIJIJI CHA KITAMA MJINI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUSIMAMIA BEI YA KOROSHO

Mkulima wa zao la korosho katika Kijiji cha Kitama Mjini kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, Selemani Awadhi akiwalipa baadhi ya wakusanyaji wa korosho katika shamba lake hapo jana (Jumamosi Novemba 17, 2018) mara baada ya kupakia bidhaa hiyo katika magunia tayari kwa ajili ya usafirishaji katika maghala ya kuhifadhia zao hilo.
................................................


WAKULIMA wa zao la korosho katika Kijiji cha Kitama Mjini Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na msimamo wa Serikali yake katika kupanga bei ya zao hilo na kuwadhibiti wafanyabiashara wasiojali maslahi ya Wakulima.

Wakizungumza na Mwandishi wa MAELEZO, Kijijini hapo jana (Jumamosi Novemba 17,2018) wananchi hao walisema hatua iliyochukuliwa na Serikali imeonesha juhudi za Rais Magufuli katika kuwasaidia wananchi wanyonge hususani wakulima ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakinyonywa na Wafanyabiashara kutokana na kununua mazao yao katika bei za chini.

Mmoja wa Wakulima hao Bw. Mohamed Aibu alisema juhudi zilizofanywa na Rais Magufuli katika kuwasaidia wakulima wa zao la korosho hazina budi kuungwa mkono na Watendaji wote wa Serikali wanaosimamia mnyororo wa thamani ya zao hilo kwani kwa sasa hakutakuwa na ukwepaji wa maagizo ya Kiongozi Mkuu wan chi.

Aliongeza kuwa zao la korosho ni miongoni mwa zao muhimu la kibiashara kwa wakulima wengi wa Mikoa ya Kusini ikiwemo  Mtwara na hivyo kuiomba Serikali kuendelea kuweka mkazo katika usimamizi na ufuatiliaji wa bei ya zao hilo kila msimu wa kilimo cha zao hilo unapoanza.

Naye Bi. Ashura Sefu anasema wananchi wa kijiji hicho wamefurahishwa na hatua ya kiutendaji iliyochukuliwa na Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujumla kwani kutawaongezea ari na nguvu katika kuzalisha korosho bora zinazokidhi masoko ya ndani na nje ya nchi.

Aidha aliiomba Serikali kujenga kiwanda cha kubangulia korosho za wakulima hao katika kijiji hicho, kwani kulingana na takwimu zilizopo kijiji hicho ni moja ya vijiji vinavyoongoza kuzalisha korosho katika Wilaya hiyo.

Kwa upande wake Selemani Awadhi anasema tamko lilitolewa na Rais Magufuli litaamsha amri kwa wadau wa tasnia ya zao la korosho kuendelea kuzalisha korosho zilizozingatia viwango na ubora wa masoko ya ndani na nje, na hivyo kuiomba Serikali kuendelea kuwekeza katika utafutaji wa masoko na pembejeo.

Saturday, November 17, 2018

TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Fransis Msungu akiongea kwenye semina iliyowashirikisha watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu kutoka halmashauri za jiji na wilaya ya Arusha sanajri na wakuu wa vituo vya polisi wilayani hapa iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha zote na mahmoud ahmad arusha.
......................................

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi na kuondoa malalamiko kutopata huduma stahiki.

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo iliyowashirikisha watendaji wa mitaa,Kata, Wakuu wa vituo vya polisi,waalimu wakuu wa shule sanjari na watumisha wa idara za serikali wilayani hapa Meneja wa mamlaka hiyo
 Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.

Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya wizi wa mtandao.

“Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa

Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.
Muwasilishaji kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini Tcra Janny Kaaya akitoa mada wakati wa semina ya watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu na wakuu wa vituo vya polisi walioshiriki semina hiyo kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha na mahamoud ahmad wa globu ya jamii arusha
Katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini David Mwakiposa akifunga semina hiyo iliyowashirikisha Halmashauri za jiji la Arusha na wilaya ya Arusha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Rose jijini hapa picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha.

Thursday, November 15, 2018

MENEJA DAWASA BAGAMOYO AAHIDI KUPOKEA MRADI WA MAJI VIKAWE

NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

MENEJA wa mkoa wa mamlaka ya maji safi na salama (DAWASA) wilayani Bagamoyo ,mkoani Pwani, Alex Ngw’andu ameahidi kuwa wataupokea mradi wa maji kutoka Ruvu Chini -Vikawe Shuleni  -Miwale Kibaha Mjini , ifikapo novemba  30 mwaka huu. 

Ametoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kuunda kamati ya watu sita wiki iliyopita, kwenda kwake kufuatilia suala hilo ili kuondoa kero ya kipindi kirefu ya ukosefu wa maji kwa wakazi wa Vikawe. 

Ngw ‘andu alisema ,kamati hiyo imefika ofisi kwake kwa nia ya kujua kama DAWASA itauchukua mradi wa Vikawe  kutokana na halmashauri ya Mji huo kuonekana kushindwa kuuendesha mradi ipasavyo.

Alieleza, tayari Bagamoyo wameshaupitia mradi na wahandisi wameshapata michoro na taarifa za uendeshaji na sasa wanajiaandaa kuufufua kwa maana kuweka umeme wa uhakika ili pampu za kusukuma maji zifanye kazi masaa angalau16 kwa siku.

“Kufufua vizimba (DP) vilivyopo na kuanza house connections (kusambaza majumbani) kwa wateja ifikapo January 2019 “
“Kwa ufupi ni kwamba mradi utapokelewa end of this month, maji na huduma iliyokuwa inatolewa awali itakuwa restored, ikiwa ni pamoja na maboresho ya kipindi cha upatikanaji maji”,alifafanua Ngw’andu.

Alieleza, wamekubaliana na kamati hiyo maalumu ya mbunge Koka yenye diwani wa eneo la Pangani,  wahandisi na msaidizi wa mbunge kuwa DAWASA pia itakwenda kutembelea eneo la huduma Vikawe jumamosi ijayo.

Kwa upande wake ,katibu wa mbunge Method Mselewa alimshukuru meneja huyo kwa kushughulikia kero za wananchi. 

Mselewa alisema, kwa hakika DAWASA ya sasa inakwenda kujibu kero ya ukosefu wa maji Vikawe ambayo ilikuwa ikisababisha wakazi wa eneo hilo kutumia maji ya visima licha ya kuwa mjini.

MBUNGE WA TEMEKE (CUF) AJIUZULU UBUNGE

Mbunge wa TEMEKE (CUF), Abdallah Mtolea amejivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya CUF akidai kumekuwa na migogoro mingi ndani ya chama chake. Mtolea ametangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma hii leo Novemba 15, 2018.

Baada ya kumaliza kutangaza kujiuzulu, Mtolea alitoka nje ya Ukumbi wa Bunge na kuondoka bungeni hapo.

Taarifa hizo zimethibitishwa pia na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ambaye amesema amepokea barua ya kujiuzulu kwake.

Aidha, Mtolea amevikaribisha vyama vingine vya siasa nchini kufanya naye kazi akidai bado anatamani kuendelea kuwatumikia wananchi wa Temeke.

SERIKALI YAOMBWA KUTOA ELIMU KUHUSU ZAO LA MKONGE.

Naweed Mulla mwenye kofia ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Highland Estate akimuonyesha mbunge wa chalinze jinsi mkonge unavyofanyiwa hatua mpaka kufikia mwisho kwa kusafirishwa.
...................................................

Na Shushu Joel,chalinze.
SERIKALI  imeombwa kutoa elimu kwa wananchi wote nchini ili waweze kulima zao la mkonge kama wanavyolima mazao mengine ya biashara  kwa manufaa yao katika kujiongezea kipato.
Rai hiyo imetolewa na Naweed Mulla   mkurugenzi wa kampuni ya Highland Estates Limited inayojishughulisha na ulimaji wa na uuzaji wa zao la mkonge, iliyoko katika halmashauri ya chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani alipokuwa akizungumza na mbunge wa jimbo hilo mara baada ya kutembelea kiwandani hapo.
Alisema kuwa endapo wananchi watahamasika kulima mkonge hapa nchini basi zao hili litazidi kupanda thamani  na kuongeza tija kubwa katika kilimo cha mazao ya biashara na hata kuachana na kulima mazao mengine kutokana na zao hilo kuwa katika nafasi za juu hapa duniani.
 “Zao la mkonge ni utajiri uliojifichaambao wananchi wa tanzania asilimia kubwa hawajatambua thamani ya zao hilo ila kwa haraka haraka ni zao lenye mafanikio ya haraka kwa wakulima “Alisema Mulla
Aliongeza kuwa kama serikali ikitoa elimu kwa wakulima na kutilia mantiki kwa wakulima kila mmoja kulima angalau ekali 3 za mwanzo ili waweze kuona manufaa yake hivyo watanzania watalima mkonge kwa wingi.
Naye ....ni moja ya wafanyakazi  katika kiwanda hicho anaeleza kuwa kiwanda hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wao na wananchi walio karibu na eneo hilo katika nyanja mbalimbali ya kijamii.
Aliongeza kuwa sitahiki zote zinazohitajika kwa watumishi zinatolewa na kiwanda hicho ila tu kulingana na kiwango chako cha elimu na uzoefu katika nafasi hiyo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa kuna haja ya serikali kuhamasisha zao hili nchini ili kuwanufaisha wakulima wadogo wadogo kutokana na hali halisi ya uhitajikaji wake kuwa mkubwa katika nchi zilizoendelea.
Aliongeza kuwa kiwanda hicho cha Mkonge kinahitaji mikonge ya kutosha hivyo wananchi wakilima zao hilo litawasaidia katika kujipatia kipata na kuweza kufanya maendeleo mengine.
Aidha mbunge huyo amempongeza mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa jinsi anavyowajali watumishi wake kwa kuwapatia mahitaji sitahiki na kwa wakati kwani hakuna llamiko alilopewa kuhusu unyanyasaji kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.
“Nimetembelea  kiwanda hicho ili kujionea uzalishaji wa zao la mkonge na hatua zake za upatikanaji wake nimejifunza vitu vingi lakini kikubwa ni kuwahamasisha wananchi kulima zao la mkonge kitu ambacho kitawafanya wakulima kujiongezea kipato” Alisema Ridhiwani.
Pia ameipongeza kampuni hiyo kwa jinsi inavyijitolea katika ufanikishaji wa miradi ya kimaendeleo kwa wananchi walio jirani na kiwanda hicho kwa kuwajengea zahanati,majengo mawili ya madarasa na mambo mengine mengi kwa kusudi la kuwasaidia walio kwenye mazingira ya karibu.
 
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Highland Estate Limited Naweed Mulla wakiangalia mkonge ulioanikwa.
 
Mbunge Ridhiwani akiangalia hatua za mwisho za zao la mkonge mara baada ya hatua zote kufanyika hapo sasa tayari kwa kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya mauzo.

DC NEWALA AKAMATA KOROSHO KUTOKA MSUMBIJI

Siku moja tu baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Joseph Magufuli kutangaza kuwa Serikali itanunua korosho kwa Bei Tshs 3300/= kwa kilo moja na Zoezi kusimamia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huku akipiga Marufuku Uingizwaji wa korosho kimagendo kutoka nje ya Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe Aziza Mangosongo amemkamata Mtu Mmoja akiingiza Korosho kimagendo Magunia zaidi 90 yenye kilo zaidi 100 kila moja katika Maeneo ya Mpakani akivusha korosho Wakati wa Operation Maalumu inayoendelea Wilayani humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama, Wilaya ya Newala, Mhe Aziza Mangosongo akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo Pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Newala katika Operesheni Hiyo.

“Mhe Aziza ametoa wito kwa wananchi waendelee kutoa Ushirikiano kwa Serikali kuendelea kufichua Vitendo Vichafu kutaka kuihujumu nchi na Ukiukwaji wa Sheria.”

WAZIRI UMMY AAGIZA KUANZISHWA DAWATI LA JINSIA, WATOTO NA WATU WENYE ULEMAVU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea Mikakati mbalimbali ya Serikali katika kumuwezesha mwanamke mlemavu  katika kongamano la Siku ya Wanawake wenye Ulemavu nchini iliyofanyika jana Novemba 14, 2018 Jijini Dodoma kwa kuandaliwa na Taasisi ya IKUPA Trust Fund.
...........................................

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza uanzishwaji wa Dawati la Jinsia, Watoto na Wenye ulemavu katika vituo vya polisi nchini.

Ameyasema hayo jana Novemba 14, 2018  jijini Dodoma wakati akizungumza katika Kongamano la Siku ya Wanawake wenye ulemavu nchini yenye lengo la kuwawezesha wanawake wenye ulemavu.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imedhamiria kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wenye ulemavu nchini na sasa imeanzisha Dawati hilo.

“Tunalo Dawati la Jinsia katika Jeshi la Polisi ila kutokana na changamoto za wenzetu walemavu naomba Dawati hilo libadilike na liwe ni Dawati la Jinsia, Watoto na watu wenye ulemavu” alisisitiza Mhe. Ummy.

Pia Waziri Ummy  pia ametoa onyo kwa waajiri kutoka Taasisi za Serikali na binafsi watakaowanyima ajira watu wenye ulemavu kwa makusudi kwani hatua kali zitachuliwa dhidi yao.

Waziri Ummy amesema kuwa walemavu wenye sifa stahiki za kupata ajira sharti wapewe ajira wasibaguliwe kutokana na ulemavu wao.

Mhe. Ummy amesisitiza uwezeshaji kwa watu wenye walemavu hasa wanawake na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutoa mikopo yenye tija.

“Niwatake wakurugenzi wa Halmashauri kutoa mikopo yenye tija na sio laki mbili kwa kikundi kimoja ili kuofanikisha azma ya kuwezesha kiuchumi wanawake hasa wenye ulemavu” alisisitiza Mhe. Ummy.

Waziri Ummy pia amemuagiza Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kuratibu uwepo wa uwakilishi wa wanawake wenye ulemavu katika majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika ngazi mbalimbali ili kutoa fursa sawa kwa wanawake wote.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju amesema kuwa Wizara inayosimamia masuala ya Afya inatakiwa kuanzisha chumba maalum kwa ajili ya wanawake wenye walemavu kujifungulia na kuruhusu wanawake hao kuja na wasaidizi katika vituo vya Afya na Hospitali.
 
“Naomba Mgeni rasmi hili liko ndani ya uwezo wako Wanawake wenye ulemavu wapate nafasi pekee ya kupata huduma za Afya ya Uzazi” alisisitiza  Bw. Mpanju

Aidha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kuziona changamoto za watu wenye ulemavu hasa wanawake na kuanzisha Kongamano ambalo litaleta changamoto ambazo zitasaidia kuleta majibu ya utatuzi wake yatakayowezesha ustawi wa walemavu nchini.

“Awamu hii ya Tano imekumbuka sana watu wenye ulemavu kwa kutoa fursa kwa kundi hili kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi naipongeza Serikali yetu” alisisitiza Dkt. Tulia.

Dkt. Tulia ameleza kuwa changamoto za watu wenye ulemavu hasa kwa watoto wenye ulemavu na katika fursa za mikopo, ajira elimu na sekta nyingine  uzingatie hasa mahitaji maalumu ya walemavu.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Watu wenye ulemavu Mhe. Ikupa Stella Alex amewashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi yake ya Ikupa Trust Fund kwa kuwezesha kongamano la  Wanawake wenye Ulemavu kwani inahimiza Serikali na wadau kuzingatia changamoto zinazowakabili walemavu hasa wanawake.

Mhe. Ikupa ameongeza kuwa suala la watu wenye ulemavu lizingatiwe kwani ni kundi lenye changamoto nyingi hivyo tunahitaji ktoa kipaumbele katika kuwapa huduma stahiki. 

Nao baadhi ya wanawake wenye ulemavu nchini wameiomba Serikali kuendelea kuweka miundombinu rafiki itakayowezesha walemavu kupata huduma rafiki katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya.

Kongamano la wanawake wenye ulemavu 2018 limeadhimishwa ikiwa na Kauli mbiu isemayo “Haki sawa za Wanawake wenye Ulemavu katika kufikia Maendeleo Jumuishi ikiandaliwa na kuratibiwa na Shirika la Ikupa Trust Fund.
 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Watu wenye ulemavu Mhe. Ikupa Stella Alex akiwashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi yake ya Ikupa Trust Fund kwa kuwezesha kongamano la  Wanawake wenye Ulemavu lililofanyika Jijini Dodoma kwa kuandaliwa na Taasisi ya yake ya Ikupa Trust Fund.

 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na mmoja wa wanawake mlemavu mara baada ya kushiriki kongamano la  Wanawake wenye Ulemavu lililofanyika Jijini Dodoma kwa kuandaliwa na Taasisi ya yake ya Ikupa Trust Fund.

Baadhi ya wanawake wenye ulemavu walioshirki kongamano la  Wanawake wenye Ulemavu lililofanyika Jijini Dodoma kwa kuandaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu( hayupo pichani)  akielezea Mikakati mbalimbali ya Serikali katika kumuwezesha mwanamke mlemavu  katika kongamano la Wanawake wenye ulemavu nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(katikati)  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson( wa pili kulia)  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Watu wenye ulemavu Mhe. Ikupa Stella Alex (kulia)  na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amos Mpanju (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake wenye ulemavu mara baada ya kumalizika kwa kongamano la  Wanawake wenye Ulemavu lililofanyika Jijini Dodoma kwa kuandaliwa na Taasisi ya yake ya Ikupa Trust Fund.

DC. DODOMA MJINI AKAMATA WALA UNGA MITAANI.


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, akiwa mtaani kukamata watumiaji wa dawa za kulevya.
.......................................... 
Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, amefanya operation ya kushtukiza katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dodoma  na kuwa baini vijana wanaotumia madawa ya kulevya aina ya gundi tatizo ambalo limekuwa sugu katika Jiji la Dodoma.

Katika operation hiyo Katambi amefanikiwa kuwakamata vijana ambao wamekuwa wakitumia madawa hayo ambayo yamekuwa yakiwaathiri vijana kwa kiasi kikubwa kwani gundi hiyo wakivuta imekuwa ikiwalewesha.

Hata hivyo waathirika wa madawa hayo wamemuonesha mahali ambapo wamekuwa wakinunua madawa hayo, na Mkuu wa Wilaya kuweka mtego wa kuwanasa wauzaji hao, kwa kuwatuma watumiaji hao na kufanikiwa kumkamata muuzaji wa duka hilo Veronica Valerian, pamoja na mmiliki wa duka hilo Hechikael Valerian.

Hata hivyo Mmiliki wa duka hilo aliwakana vijana hao kwa kudai kuwa hawafahamu wala hajawahihi kuwauzia gundi, mara baada ya kufikishwa katika kituo cha cha polisi kati Dodoma, wauzaji walikili kuwauzia watoto hao, lakini wakidai mmiliki wa duka alikuwa hatambui biashara hiyo.

“Ni kweli tunawauzia gundi lakini mama hatambui ndio maana alikataa kutambua biashara hiyo na alikuwa hatambui chochote kuhusu swala hili na hakuona biashara hiyo.” Alisema Veronica.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Patrobas Katambi amesema ameamua kufanya operation hiyo baada ya kuona vijana wadogo wanateketea katika janga hilo la uvutaji gundi ambalo limekuwa likiathiri watoto wengi hapa mjini.

“ Nimeamua kufanya operation hii kwa sababu nimeona vijana wengi hapa mjini wanateketea katika janga  hili na tusipo chukua hatua watoto wetu wataharika zaidi, sababu janga limekuwa kubwa.” Alisema Katambi.

Amesema na vijana wengi walioingia kwenye janga hili si wakazi wa Dodoma, bali ni wale waliotoka nje ya Dodoma, waliokuja kutafuta maisha lakini kutokana na umri wao kuwa mdogo wanakosa fursa hali inayowapelekea kuingia katika janga la uvutaji wa madawa ya kulevya.

Amesema vijana hawa hununua gundi na kuiweka kwenye vikopo na kuanza kuivuta hali inayopelekea vijana hawa kulewa, na ukivuta gundi hii inapelekea kuhalibu mfumo wa fahamu na kupoteza uwezo wa kufikili na kupelekea  kuhalibika na kuwa vibaka mitaani.

Vilevile amezitaka jamii kulichukulia kwa uzito swala hili kwa sababu ni kinyume na maadili yetu  na kinyume na sheria za Nchi yetu kwahiyo kila mtu anawajibu wa kuzuia vitendo hivi.