MANISPAA TABORA YAASWA KUONGEZA MAPATO
MANISPAA TABORA YAASWA KUONGEZA MAPATO Na Allan Kitwe, Tabora HALMASHAURI ya Manispaa Tabora imetakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato katika vyanzo vyake ili kufanikisha utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata zake zote. Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella alipokuwa akizungumza na watalaamu, watendaji, madiwani, viongozi wa chama, wawakilishi wa taasisi na vyombo vya ulinzi na usalama. Wella ameeleza kuwa licha ya kwamba serikali inapeleka fedha nyingi katika halmashauri zote kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo, halmashauri hazipaswi kubweteka, zinatakiwa kujiongeza kwa kukusanya mapato zaidi. ‘Mapato ya halmashauri ni muhimu sana kwa kuwa yanasaidia kuharakisha utekelezaji miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kukamilisha miradi yote inayoanzishwa katika kila kata’, amedokeza. Amesisitiza kuwa kusuasua kwa baadhi ya miradi katika vijiji, mitaa na kata kunachagiwa na ufinyu wa bajeti lakini kama halmashauri it...