Saturday, May 23, 2020

TPDC YAWALIPA FIDIA WANANCHI LINDI.

No description available.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la maendeleo ya petrol Tanzania  (TPDC) Dr. James Matarangio katikati akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi  Bilioni 2.036 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kulia kwake kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wa Mto mkavu ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Gesi asilia (LNG) na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano TPDC,  Marie Msellemu
...............................................

Na HADIJA  HASSAN, LINDI.

SHIRIKA  la Maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC limekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi  693 wa Mtaa wa Likong’o, Masasi ya leo na Mto mkavu ili kupisha Mradi wa kiwanda cha uchakataji wa Gesi asilia (LNG)  katika kata ya Mbanja  Manspaa ya Lindi Mkoani humo kwa kukabidhi  mfano wa hundi ya shilingi bilioni 5.2.

Akizungumza  wakati wa kukabidhi hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania  TPDC , Dr.James Mataragio kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi alisema kuwa  kati ya hizo Bilioni 5.2, bilioni  2.3 zitalipwa kwa wananchi wa Mtaa wa Likong’o na Masasi ya leo huku  bilioni 2.036 zitalipwa kwa Wananchi wa Mtaa wa Mto mkavu.

Dkt. Mataragio Alisema mpaka sasa zoezi hilo limekamilika kwa asilimia 88 ambapo Wananchi wapatao 617 kati ya 693 wameshasaini mikataba ya makubaliano baina yao na TPDC tayari kwa kulipwa fedha zao huku Wananchi 76 waliosalia wakiwa bado hawajakamilisha taratibu na nyaraka zao  zipo kwenye ukaguzi.

Aidha Dr, Mataragio aliongeza kuwa  zoezi hilo la utowaji wa Mfano wa  hundi linaenda sambamba na ulipaji wa fidia kwa wananchi ambapo mpaka sasa tayari wananchi mia tatu (300)  wa awamu ya kwanza wameshaingiziwa fedha zao Bank.

Hata hivyo Dkt. Mataragio alieleza kuwa hatua hiyo ya ulipaji wa fidia ni miongoni mwa mwendelezo wa hatua za  ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa cha uchakataji wa Gesi asilia (LNG) ambao utagharimu Dolla za kimarekani bilioni 30.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano huo wa  Hundi pamoja na kulipongeza Shirika hilo kwa kuendesha zoezi la ulipaji wa fidia  kwa uwazi pia alitoa onyo kwa wataalamu pamoja na wananchi wajanja wajanja kuanza kupeleka madai yasiyo kuwepo.

“kuna watu watakuja kufungwa hapa kwa sababu ya tamaa , hapa Lindi yupo mtu mmoja kila madai na migogoro ya Aridhi inapokuja nayeye lazima awepo kila mtaa yeye yupo tu sasa najiuliza huyo mtu kila mtaa ni wake? Kwa hivyo na hapa napigia hesabu tukiwaona watu kama hao tutawafunga” alitaadharisha Zambi.

“lakini pia niwaonye na wataalamu wetu wakati mwingine ipo tabia pia ya kuweka majina ya watu ambao hawakuwepo, majina hewa. Tusije tukaona majina hewa, na nadhani tulifanya pia vizuri ya  kuhakikisha kwamba kila mtu anakuja hapa anasimama  na anapiga picha mwenyewe” aliongeza Zambi.

Hata hivyo zambi alitilia mashaka kwa watu 76 ambao hawakujitokeza katika zoezi hilo huwenda yalikuwa ni majina hewa yaliyotengenezwa na wataalamu wa maeneo hayo ambao kulingana na uendeshaji wa zoezi lenyewe walishindwa kuwapata.

Mwalimu kibogoyo ni mmoja ya wa wananchi walioathirika na mradi huo ambapo pamoja na kukili kuingizia fedha yake ya fidia kwenye Ankaunt yake pia aliliomba shirika hilo kutoa muda wa kutosha ili wananchi wanaopisha mradi wapate muda wa kutosha wa kufanya maandalizi mapya ya makaazi yao mapya.

DKT. KAWAMBWA AKABIDHI FUTARI KWA WASIO NA UWEZO BAGAMOYO.

No description available. 
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wahisani  Doris mollel foundation Tika kutoka nchini Uturuki, kwa pamoja wakikabidhi futari kwa wanachi wasiojiweza katika jimbo hilo.
.......................................

Na SELESTIAN JAMES.

Taasisi ya Doris mollel foundation kwa kushirikiana na taasisi ya Tika kutoka nchini Uturuki zimetoa mifuko mia moja na hamsini ya  sadaka futari kwa waumini wa dini ya kiislamu walio katika makundi maalum katika maeneo ya Kiromo kitopeni na hospitali ya Wilaya Bagamoyo, wilayani Bagamoyo.

Akizungumza hivi karibuni muwakilishi wa taasisi ya Doris mollel foundation. Doris Mollel amewashukuru taasisi ya Tika kwa kuwaunga mkono kwa mara nyingine katika utaratibu wa kugawa futari ambao huwa wanaufanya kila mwaka, katika kusaidia waislamu hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali akiwemo mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa na diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga, imewawezesha waumini wa dini ya kiislamu katika kata hiyo kupata sadaka ya futari kwenye mifuko iliyokuwa na maharage, mchele, sukari, chumvi, tambi, na mafuta.

Kwa upande wake, muheshimiwa Mbunge Dkt. Kawambwa amezishukuru tasisi hizo kwa niaba ya wananchi wa Bagamoyo kwa kuona umuhimu wa kutoa sadaka hizo jimboni humo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo huo wa kuwasaidia watu wasiojiweza katika mambo mbalimbali na kuwaombea mungu awazidishie kwa kila jema wanalolifanya.

Amewaomba waumini hao wa dini ya kiislamu kuziombea  taasisi hizo ziweze kufanikiwa katika shughuli zao za kila siku ili waendelee kutoa faraja kwenye jamii mbalimbali.

Kwa upande wao wanumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanufaika na msaada huo wa futari wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Bagamnoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kwa kuwaletea wafadhili wa kuwa futari.

Wamesema wao wasingewajua wafadhili hao na kwamba mbunge angeamua kuwapeleka popote lakini kuwachagua wao watu wasiojiweza ni huruma yake na kuonyesha namna anavyowajua watu wa jimbo lake.

Aidha, viongozi na waumini waliokuwepo katika maeneo hayo wamewaombea dua ya shukurani  kuwatakia safari njema na kuwakaribisha siku nyingine wanapokuwa na sadaka mbalimbali basi wasisite kufika maeneo hayo.
No description available. 
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (wa pili kushoto) akipanga maboksi ambayo ndani yake kuna maharage, mchele, sukari, chumvi, tambi, na mafuta, vilivyotolewa  na wahisani  Doris mollel foundation naTika kutoka nchini Uturuki.
No description available. 
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (kushoto) akiwaweka sawa wananchi wake kwaajili ya kuwapatia msaada wa futari iliyotolewa na wahisani  Doris mollel foundation naTika kutoka nchini Uturuki.
No description available. 
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, (kushoto) akijadiliana na Diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga.
No description available.
 Baadhi ya walengwa wa msaada wa futari hiyo.
No description available.

Thursday, May 14, 2020

Masoud Kipanya, Shishi baby waukwaa ubalozi wa naweza, watoa nasaha nzito kwa wazazi













Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa wazazi wanapaswa kujiona ni wenye bahati kwa kupata mtoto na kwamba wanatakiwa kumthamini kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kumpa stahiki zake zote ikiwemo kumnyonyesha kwa miaka miwili bila kumkatisha.

Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la mawasiliano la naweza kupitia smart generation, Shilole alisema kuna wanawake wengi sana wamekuwa na tabia ya kikatili ya kumnyima mtoto wake kunyonya kwa muda mrefu, wakihofu usichana wao utakwisha.

Alisema jambo hilo sio zuri, kupitia jukwaa la naweza atahakikisha anahamasisha wanawake kuwa na tabia ya kuwathamini watoto wao, waache tabia ya kuwawekea pilipili katika chuchu mara tu inapofika miezi mitatu.

“Mthamini mtoto wako, usimkatili mtoto ndani ya miezi mitatu unamnyima ziwa huko ni kumkosea mtoto, lakini pia ni kujitengenezea mtoto ambaye hana akili, anakuwa zezeta,” alisema Shilole.

Usiogope kuwa ziwa litadondoka, ukishakubali kuwa mama huna sababu ya kuwaza kuwa ziwa lako linadondoka, hakikisha unampa haki zake

 

Kwa upande wake balozi Masoud Kipanya, aliwaasa wanaume kuhakikisha mama anasaidiwa katika kila hatua ya makuzi ya mtoto.

Alisema ni vizuri wakina baba kuwa mstari wa mbele katika ustawi wa mtoto.

“Baba bora ni pamoja na kuhakikisha mtoto unamsimamia vya kutosha, idadi ya vifo 30 kwa siku vinavyotokana na uzazi inaweza kupungua kama tutajitahidi kuwa sehemu makuzi ya mtoto.

 

Kwa upande wake mtaalam kutoka taasisi ya 360 fhi Bw. John Bosco akielezea mradi wa naweza ambao uko ndani ya mradi wa USAID tulonge afya, alisema naweza ni jukwaa la mawasiliano la kubadilisha tabia, ni jukwaa ambalo linampa mtanzania uhakika wa afya yake ya kesho, linamuwezesha baba kuwa baba bora,

Kuwa baba bora ni pamoja na kuwa karibu wakina mama, kuwahamasisha kwenda kliniki, kuwasindikiza kwenda katika kituo cha afya, unaweza kuwa baba bora au mama bora kupitia jukwaa la naweza

Jukwaa la naweza linaanza safari na mama wakati anapoanza kushika ujauzito, linamkumbusha mama kwenda kliniki, kutumia chandarua chenye dawa, kutumia vidonge vinavyomkinga mtoto dhidi ya malaria, kunyonyesha mtoto, kutumia njia ya afya ya uzazi ili kumkuza mtoto vizuri, linawakumbusha wenzi kuwa na tabia chanya ya kumlinda mtoto.

Naweza wanambinu mbalimbali ya kuwafikia jamii, lakini kutokana na ugonjwa wa corona wamejikita zaidi katika mitandao ya kijamii. Ni jukwaa la mawasiliano kwa lengo la kubadilisha tabia.

Mabalozi wa jukwaa la naweza,

Kutokana na umuhimu wa kazi ya jukwaa la naweza viongozi wameamua kuteuwa mabalozi wa jukwaa hilo ili kufikisha ujumbe mbali zaidi, waliobahatika kuwa mabalozi hao ni pamoja na msanii maalufu, Shilole na Mtangazaji, Masoud Kipanya.

 

Siza “Tumekuwa tukipokea maswali mengi sana kuhusu mradi ambao tumeuzindua wiki iliyopita, mradi wa kuingiza vitabu nchini Tanzania, vitabu laki moja, ambao tulisema tulisaini makubaliano na wenzetu kutoka nchini Uingeleza wa kuingiza vitabu kati ya 20,000 hadi 30,000 kila mwezi

Habari njema ni kwamba wiki ijayo tunauzindua rasmi mradi huo na vijana wengi tunategemea wanapata fursa mbalimbali ikiwemo namna ya kushirikiana nao juu ya kusaidia biashara zao, ambao hawana mitaji ya kutosha,

 

Wednesday, May 13, 2020

WANAKIJIJI RUTAMBA HALMASHAURI YA MTAMA KUONDOKANA NA SHIDA YA MAJI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

HATUA  ya Serikali kupitia wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Lindi Mkoani humo kufanya ukarabati wa mradi wa maji katika kijiji cha Rutamba halmashauri ya Mtama kinaelezwa kitasaidia kunusuru Ndoa za wakazi wa kijiji hicho

Mradi huo ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 340 unatekelezwa kupitia mpango wa PFR (Payment for Result) kwa kutumia mafundi wa kawaida na umeanza kutekelezwa rasmi 22/04/2020 na unatarajiwa kukamilika  tarehe 30/06/2020

Akieleza  matumaini yake Mwanaidi Saidi Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho   mbele ya kamati ya ulinzi na usalama  ya wilaya hiyo iliyofika katika kijiji hicho ili kujionea maendeleo ya mradi huo, alisema kuwa  kinamama wa maeneo hayo  hutumia muda mwingi kuhangaika kutafuta maji hali ambayo inawafanya waume zao kukosa imani kwa  wanawake hao

“Kwa kweli swala la maji ni pigo sana kwa kina mama kwa sababu  yani mama mpaka saa sita ya usiku hajalala anasubiri maji  na kwa vile maji yalikuwa hayatoki tulikuwa tunaenda mtoni  ambako ni mbali na kijiji kilipo  ambako pia tulikuwa tunalazimika kutoka  saa kumi alfajiri ili tuweze kuwahi kufika  na kuchota maji na kuondoka” Alisema Mwanaidi.

“Kwa kuwa sasa maji yanatoka na kukatika  kwa muda  wa usiku, kwa hivyo  kinamama tunakaa kwenye vile  vilula  kuanzia saa mbili ya usiku  mpaka saa sita na wakati mwingine maji tunakosa, kiasi kwamba tunakata tama tunaamua kwenda kulala tuamke tuu saa kumi ili twende mtoni tukafuate maji”


Mwanaidi alisema  Hali hiyo inawafanya waume  walio wengi wa maeneo hayo  kukosa  imani kwa wanawake zao kuwa huwenda wanatumia mwanya huo wa kutafuta maji kuchepuka ndoa zao  

“Muda mwingi tunatumia kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za kimaendeleo , tunatumia zaidi ya massa sita mpaka saba kutafuta maji  mfano ukitoka nyumbani saa 10 alfajili utarudi nyumbani saa tatu au saa nne Asubuhi  tena ukiwa umepata kindoo kimoja ambacho hata hakitoshi kwa matumizi ya hapa nyumbani” alieleza mama mwingine Fatuma selemani.

Kwa mujibu wa meneja wa Ruwasa wilaya ya Lindi Iddy Pazi amesema kuwa  Mradi wa Maji Rutamba ni kati ya Miradi inayotekelezwa kupitia mpango wa PFR katika wilaya hiyo  ambayo inaghalimu kiasi cha Bilioni 100.na milioni 1

Alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa matanki mawili ya maji ya lita laki moja , vituo vinne vya kuchotea maji  (vilula) ambavyo vitakuwa na koki mbili mbili pamoja na ukarabati wa koki kumi na saba ambazo zilikuwa zikitumia awali



Nae mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga  akiongozana  na kamati hiyo akizungumza mara baada ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo alimtaka Meneja huyo wa Ruwasa kuhakikisha miradi yote anayoisimamia inakamilika kwa wakati.


SHERIA YA KODI YATOA MSAMAHA KWA MAPATO YASIYOZIDI MILIONI 4 KWA MWAKA


Na. Josephine Majura na Saidina Msangi, WFM, Dodoma.


Serikali imeeleza kuwa Sheria ya Kodi imetoa msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na wastaafu ambao mapato yao kwa mwaka hayazidi Shilingi milioni nne.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Lupembe, Mhe. Joram Ismael Hongoli, aliyetaka kujua sababu za Serikali kutoweka utaratibu wa kutowatoza kodi wastaafu ambao biashara zao hazizidi mtaji wa Shilingi milioni nne.


Dkt. Kijaji alisema kuwa wastaafu walioanzisha miradi midogo ya kilimo na biashara ambayo inawaingizia kipato kisichozidi Shilingi milioni nne hawapaswi kutozwa kodi kwa kuwa Sheria ya Kodi imetoa msamaha.

Alisema kuwa Kifungu cha nne cha Sheria ya Kodi ya Mapato kinatoa msamaha wa kodi ya mapato kwa mfanyabiashara ambaye mapato yake ghafi ya mwaka hayazidi Sh. milioni 4, hii ikiwa ni pamoja na mapato ya wafanyabiashara wastaafu ambao kiwango chao cha mapato hakizidi kiasi hicho kwa mwaka.