KAMPUNI ZA BIMA ZATAKIWA KUPANUA WIGO WA HUDUMA.
Kamishna wa Sera kutoka wizara ya fedha na mipango, Mgonya Benedicto, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango katika ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa washauri na madalali wa bima nchini uliofanyika leo tarehe 26 julai 2019, mjini Bagamoyo. Serikali imezitaka kampuni za bima nchini kuongezaa idadi ya wananchi wanaotumia bima hasa wakulima na wafugaji ili kufikia lengo la serikali la kufikisha asilimia 50 ya watu wazima wanaopata huduma ya bima ifikapo mwaka 2029. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa washauri na madalali wa bima nchini uliofanyika leo tarehe 26 julai 2019, mjini Bagamoyo. Katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kamishna wa Sera kutoka wizara ya fedha na mipango, Mgonya Benedicto, Dkt. Mpango amesema ushirikiano kati ya serikali na Kampuni za bima utaleta tija ili kuimarisha sekta ya bima hapa nchini. Alisema watanzania wengi uchumi wao...