Posts

KAMPUNI ZA BIMA ZATAKIWA KUPANUA WIGO WA HUDUMA.

Image
Kamishna wa Sera kutoka wizara ya fedha na mipango, Mgonya Benedicto, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango katika ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa washauri na madalali wa bima nchini uliofanyika leo tarehe 26 julai 2019, mjini Bagamoyo. Serikali imezitaka kampuni za bima nchini kuongezaa idadi ya wananchi wanaotumia bima hasa wakulima na wafugaji ili kufikia lengo la serikali la kufikisha asilimia 50 ya watu wazima wanaopata huduma ya bima ifikapo mwaka 2029. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa washauri na madalali wa bima nchini uliofanyika leo tarehe 26 julai 2019, mjini Bagamoyo. Katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kamishna wa Sera kutoka wizara ya fedha na mipango, Mgonya Benedicto, Dkt. Mpango amesema ushirikiano kati ya serikali na Kampuni za bima utaleta tija ili kuimarisha sekta ya bima hapa nchini. Alisema watanzania wengi uchumi wao...

Kampuni ya Puma kuendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah Mwandishi Wetu Kampuni ya Puma Energy Tanzania imesema itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi mbalimbali ikiwa ni mkakati wake wa kupunguza ajali nchini. Pia kampuni hiyo imetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa zaidi ya wanafunzi 4500 katika shule tano za msingi Jijini Dodoma huku ikiahidi kuendelea kutoa elimu hiyo na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa mabalozi kwa wengine. Akizungumza leo Julai 25 jijini Dodoma mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana,  Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah, amesema programu hiyo ya mwezi mmoja kwa jiji hilo ilihusisha mafunzo ya usalama barabarani kwa walimu 15 na wanafunzi 4500, katika shule tano “Puma Energy Tanzania imeamua kuja jijini Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa ...

Wahamiaji waliokuwa wanaelekea ulaya warudishwa

Image
Walinzi wa pwani nchini Libya wamesema jana wamewakamata wahamiaji karibu 40 ambao walikuwa wanaelekea Ulaya nje ya pwani ya bahari ya Mediterania na kuwapeleka katika vituo vya kuwashikilia ambavyo vilishambuliwa mapema mwezi huu. Msemaji wa kikosi hicho cha walinzi wa pwani Ayoub Gassim amesema boti ya mpira iliyokuwa imewachukua wahamiaji 38, wengi wao wamisri, ilizuiwa siku ya Jumanne nje ya pwani hiyo kiasi ya kilometa 65, mashariki mwa mji mkuu, Tripoli. Amesema wahamiaji walihamishiwa katika kituo cha kuwashikilia cha Tajoura. Umoja wa Mataifa umeeleza wasi wasi wake mkubwa jana kuwa wahamiaji hao wapya wamepelekwa Tajoura, ambako shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linakadiria kuwa wakimbizi 200 na wahamiaji wanashikiliwa hap

RC MAKONDA AENDELEA KUTIMIZA AHADI YA UFADHILI WA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 KUTOKA FAMILIA DUNI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 25 amepokea zaidi ya Shilingi Milioni 23 kutoka kwa wadau ambao wameguswa na kampeni aliyoanzisha ya ufadhili wa matibabu ya upasuaji moyo kwa watoto 60 kutoka familia zenye hali duni. Miongoni mwa Wadau waliomuunga Mkono RC Makonda ni Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. Sylvester Koka ambae amekabidhi hundi ya Shilingi milioni 10 kwaajili ya matibabu ya watoto 5 huku Mkurugenzi wa Dorka Catering Bi. Dorothy Kansolele akichangia milioni 6 na mkurugenzi wa kampuni ya Abe Professional Sound Bw. Abraham Ngomko akichangia Milioni 6 kwaajili ya matibabu ya watoto 3. Akipokea fedha hizo RC Makonda amezikabidhi kwa uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kueleza kuwa zitasaidia kugharamia zaidi ya Watoto10 kwenye upasuaji wa awamu ya pili. Aidha RC Makonda amewashukuru wadau wote wanaondelea kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya watoto ambao wangeweza kupoteza maisha kuto...

Makamu Wa Rais Kufungua Maonesho Ya Nanenane Kitaifa 2019 Mkoani Simiyu

Image
Na Stella Kalinga, Simiyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Mjini Bariadi kuanzia tarehe 29/07/2019 hadi 08/08/2019. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika mkutano maalum wa kutoa taarifa kwa Umma uliofanyika  Mjini Bariadi, Julai 24, 2019. Mtaka amesema Mhe Makamu wa Rais atafungua rasmi maonesho hayo Agosti Mosi, 2019 na waoneshaji mbalimbali zikiwemo Taasisi, Mashirika mbalimbali na wajasiriamali wataanza kuonesha teknolojia, huduma na bidhaa zao Julai 29, 2019 ikiwa ni maandalizi ya ufunguzi rasmi utakaofanywa na Mhe. Makamu wa Rais. “Shughuli ya ufunguzi itafanywa tarehe 01/08/2019 na Mhe. Makamu wa Rai, haya ni maonesho ambayo yatakaribisha viongozi wa Kitaifa, Agosti 03, 2019 tutakuwa na Mhe. Waziri...