Posts

KILWA WATENGA MILIONI 16 KUINUA UBORA WA ELIMU.

Image
Mwalimu Mshamu Ndandavale Ofisa Elimu vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kilwa akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG, ofisini kwake. Mwalimu Ayub Mwakatika, Mratibu Elimu Kata ya Tingi Halmashauri ya Wilaya ya kilwa Mkoani Lindi Miongoni mwa waratibu Elimu waliopatiwa Pikipiki na Mradi wa Kuinua ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ............................................   Na Hadija Omary, LINDI. Serikali Wilayani kilwa Mkoani Lindi imetenga kiasi cha Tsh. Milioni 16 kwa ajili ya kuendeleza shuguli mbali mbali zilizokuwa zikifanywa na Mradi wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ambao umekwisha muda wake ili usimamizi huo wa Ubora wa Elimu uweze kuwa Endelevu. Hayo yameelezwa na Mwalimu Mshamu Ndandavale Ofisa Elimu vifaa na Takwimu wa Wilaya hiyo kwa niaba ya Ofisa Elimu Msingi jana Ofisini kwake alipokuwa akizungumza na Bagamoyo kwanza Blog. Mradi huo wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) ulianza mwaka 2015 Ukiwa na malengo ya K...

MAHDI WA PARADISE BAGAMOYO AUWAWA NCHINI SOMALIA.

Image
Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte,wakati wa uhai wake.   Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte,wakati wa uhai wake. ..................................... Mfanyabiashara Mahad Nur Gurguurte, wa Tanzania ambae alikuwa mmiliki wa hoteli ya Paradise Bagamoyo ameuawa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia. Shambulio hilo la kujitoa muhanaga limetokea ijumaa ya tarehe 12 julai 2019 katika hoteli ya Asasey iliyopo  mji  wa bandari  wa  Kismayo nchini Somalia. Watu 26 wameripotiwa kufariki dunia katika shambulio hilo wakiwemo watanzania watatu, na wengine 56 kujeruhiwa. Miongoni mwa watanzania watatu waliofariki ni pamoja na mmiliki wa Hoteli ya Paradise ya Bagamoyo, Mahad Nur Gurguurte na wengine wawili (2). Aidha mb ali ya kupoteza Watanzania watatu, wengine waliopoteza maisha ni raia wa Kenya watatu, Wamarekani watatu, Muingereza mmoja na Mcanada mmoja. Watu walioshuhudia  wamesema  miongoni  mwa  w...

MAGAZETI YA LEO JULAI 14, 2019.

Image

BAGAMOYO: MWENYEKITI WA KITONGOJI (CHADEMA) AJIUZULU, AJIUNGA CCM.

Image
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashid Zahoro (kulia) akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya, Frank Daniel Masiaga ambae alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji  kwa tiketi ya CHADEMA. ............................. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyakahamba kata ya Kerege wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kwa tiketi ya CHADEMA, Frank Daniel Masiaga amejiuzulu nafasi yake na kutangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 13 julai 2019. Akitangaza uamuzi huo mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya CCM kata ya Kerege, Masiaga alisema ameamua kurudisha kadi ya CHADEMA na kuchukua kadi ya CCM kutokana na kile alichokiita ni kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kuleta maendeleo. Alisema katika kipindi chote cha miaka mitano amekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji kupitia Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini amefanya kazi katika mazingira magumu hivyo ameona ni bora ajiunge na CCM ili aweze kufanya ...